UCHAGUZI WA GOFU WANAWAKE KUFANYIKA APRIL 1, 2018.

Afisa Habari wa BMT Najaha Bakari akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu uchaguzi wa chama cha mchezo wa Gofu wanawake unaotarajiwa kufanyika 1 April, 2018.
Afisa Habari wa BMT Najaha Bakari akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu uchaguzi wa chama cha mchezo wa Gofu wanawake unaotarajiwa kufanyika 1 April, 2018.

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limetangaza uchaguzi wa chama cha Gofu wanawake unatarajiwa kufanyika Tarehe 1 April, 2018 katika klabu ya Gofu Lugalo Jijini Dar es Salaam..

Akitangaza uchaguzi huo mbele ya waandishi wa habari leo hii  Machi 23, 2018, katika moja ya kumbi za uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam, Afisa Habari wa BMT Najaha Bakari amesema fomu zitaanza kutolewa bure katika ofisi za Baraza zilizopo uwanja wa Taifa, na pia kupatikana katika tovuti ya Baraza ambayo ni www.nationalsportscouncil.go.tz, kuanzia tarehe 23 hadi 30 Machi mwaka 2018.

Aidha Afisa Najaha amesema usaili utafanyika siku hiyo ya uchaguzi asubuhi, halafu utafuatiwa na mkutano mkuu kasha uchaguzi wenyewe.

Nafasi zinazogombewa ni;

  1. Rais (President)
  2. Makamu wa Rais (Vice President)
  3. Katibu wa Heshima (Hon. Secretary)
  4. Mweka Hazina (Hon. Treasurer)
  5. Katibu Mshindani ( Competition Secretary)
  6. Katibu kitambo (Handicap Secretary)

Kwa upande wa sifa za wagombea ambao watajitokeza kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo, Afisa Najaha amesema kiongozi lazima awe na sifa zifuatazo:

  1. Awe ni Raia wa Tanzania
  2. Awe na uzoefu wa uongozi pamoja na taaluma za uongozi wa Michezo.
  3. Awe na ujuzi wa mchezo wa Mpira wa Magongo.
  4. Awe hajatenda kosa lolote la Jinai.

Hivyo basi kutoa wito kwa wadau wote wenye sifa na wenye nia njema ya kuendeleza mchezo wa Gofu nchini kujitokeza kwa wingi kuchukuwa fomu, ili waweze kupatikana viongozi bora.

991 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/03/23/uchaguzi-wa-gofu-wanawake-kufanyika-april-1-2018/">
RSS