MWAKYEMBE: HAKIKISHENI MNAIPEPERUSHA VYEMA BENDERA YA TANZANIA KWA KURUDI NA USHINDI..

Waziri mwenye dhamana ya Michezo Mheshimiwa dokta Harrison Mwakyembe (Mb) akikabidhi bendera kwa mmoja wa wachezaji wanaoiwakilisha nchi katika mashindano ya Jumuiya ya Madola Masoud Mtelaso ambaye ni naodha wa Mpira wa meza leo uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Timu ya watu ishirini na moja wakiwemo wachezaji 16 na makocha 5, imeagwa leo hii kuelekea katika mashindano ya jumuiya ya madola yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi tarehe 4 hadi 16 April 2018, Gold Coast nchini Australia.

Akiiaga timu hiyo katika moja ya kumbi zilizopo uwanja wa taifa jijini Dar es salaam, waziri mwenye dhamana ya Michezo Mheshimiwa dokta Harrison Mwakyembe (Mb) amewataka wachezaji ambao wanaenda kuiwakilisha nchi katika mashindano hayo makubwa duniani, kupambana kwa hali na mali ili kuhakikisha wanaipeperusha vyema bendera ya Tanzania na kurejea nyumbani na ushindi kwani ndio kiu kubwa ya watanzania kwa sasa.

“matarajio ya watanzania zaidi milioni hamsini, ni kwamba mtatuwakilisha vyema na kurudi na ushindi,na ni imani yangu kuwa mmeiva vizuri katika maandalizi mliyofanya,nawaomba mfanye kile watanzania wanachokitaka,” Alisisitiza Dkt. Mwakyembe.

Waziri mwenye dhamana ya Michezo Mheshimiwa dokta Harrison Mwakyembe (Mb) mwenye tai Nyekundu katikati hakiwa katika picha ya pamoja na viongozi, makocha na wachezaji wanaokwenda kushiriki katika mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini Australia.

Aidha Mh. Mwakyembe amesema kuwa mashindano yajayo ya kimataifa wachezaji hawatashiriki kwa mazoea au itafaki bali watashiriki kwa vigezo sanjari na kuvisisitiza vyama kuandaa mipango kazi yao pamoja na kalenda za matukio mbalimbali zitakazowasaidia kuwaandaa wachezaji wenye vigezo kushiriki katika mashindano mbalimbali na kuliletea sifa Taifa.

“tubakoelekea hatutakwenda kwa mazoea bali kwa vigezo, kama wachezaji hawana vigezo ni bora hiyo hela ya kugharamikia safari hiyo tukanunue madawati ili watoto wasome mashuleni,”Alisema Dkt. Mwakyembe.

Kwa upande wake mmoja wa wachezaji wa mchezo mpira wa meza, Masoud Mtalaso akiongea na waandishi wa Habari kwa niaba ya wachezaji wenzake amesema watapambana vizuri ili kuhakikisha wanajerea na ushindi kikubwa tu ni dua za watanzania zinaitajika ili waweze kufanya vizuri.

“tunawaomba watanzania wote mtuombee, nasi tutapambana kuhakikisha kuwa tunarejea nyumbani na ushindi,”alisema Masoud.

1,399 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/03/28/mwakyembe-hakikisheni-mnaipeperusha-vyema-bendera-ya-tanzania-kwa-kurudi-na-ushindi/">
RSS