NEEMA: VYAMA TUMIENI MICHEZO KUTOA ELIMU KWA JAMII

Afisa Michezo wa BMT Bi. Neema Msitha akikipongeza chama cha (ATT) kwa kupiga hatua zaidi sio katika masuala ya Michezo tu, bali ata kutoa elimu katika jamii, jambo ambalo linapaswa kuigwa na vyama vingine vya Michezo nchini, kuhakikisha vinatumia vizuri Michezo kuweza kutoa Elimu katika Jamii
Afisa Michezo wa BMT Bi. Neema Msitha akikipongeza chama cha (ATT) kwa kupiga hatua zaidi sio katika masuala ya Michezo tu, bali ata kutoa elimu katika jamii, jambo ambalo linapaswa kuigwa na vyama vingine vya Michezo nchini, kuhakikisha vinatumia vizuri Michezo kuweza kutoa Elimu katika Jamii

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limekipongeza chama cha mbio za magari nchini (AAT) kwa kuzindua awamu ya pili ya mradi wa kuelimisha wanafunzi juu ya matumizi sahihi ya alama za barabarani uliozinduliwa leo hii 5 April 2018, katika shule ya mafunzo ya udereva AAT upanga jijini Dar es salaam.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja katika uzinduzi huo, Afisa Michezo wa BMT Bi. Neema Msitha amesema chama cha (ATT) kimepiga hatua zaidi sio katika masuala ya Michezo tu, bali ata kutoa elimu katika jamii, jambo ambalo linapaswa kuigwa na vyama vingine vya Michezo nchini, kuhakikisha vinatumia vizuri Michezo kuweza kutoa Elimu katika Jamii, ili Taifa liweze kusonga mbele katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo.

“Nikipongeze sana Chama cha (AAT) kwa jitihada kubwa zinazofanyika sio katika Michezo tu, bali ata katika Jamii, wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu mashuleni, juu ya matumizi sahihi ya alama za barabarani, na nadhani jambo hili linapaswa kuwa mfano wa kuigwa na vyama vingine vya michezo nchini,ili kuhakikisha Taifa linasonga mbele katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo,”Alisema Bi. Neema.

Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa (AAT) Yusuf A. Ghor akizungumzia kuhusu awamu ya kwanza ya mradi huo uliofanyika mwaka jana 2017, ambapo zaidi ya walimu 1000, kutoka shule na vyuo zaidi ya 50 walipatiwa elimu ya matumizi sahihi ya alama za usalama barabarani.
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa (AAT) Yusuf A. Ghor akizungumzia kuhusu awamu ya kwanza ya mradi huo uliofanyika mwaka jana 2017, ambapo zaidi ya walimu 1000, kutoka shule na vyuo zaidi ya 50 walipatiwa elimu ya matumizi sahihi ya alama za usalama barabarani.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa (AAT) Yusuf A. Ghor amesema awamu ya kwanza ya mradi huo ulifanyika mwaka jana 2017, ambapo zaidi ya walimu 1000, kutoka shule na vyuo zaidi ya 50 walipatiwa elimu ya matumizi sahihi ya alama za usalama barabarani, lengo likiwa ni walimu hao kuandaa mipango thabiti ya kufundisha elimu hiyo katika shule zao, jambo ambalo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

“Awamu ya kwanza ya mradi huu ulifanyika mwaka jana 2017, ambapo zaidi ya walimu 1000, kutoka shule na vyuo zaidi ya 50 walipatiwa elimu ya matumizi sahihi ya alama za usalama barabarani, lengo likiwa ni walimu baada ya kupata mafunzo kuandaa mipango thabiti ya kufundisha elimu hii katika shule zao, na tunashukuru kwa kiasi kikubwa jambo hili limefanikiwa,”Alisema Ghor.

Afisa Michezo wa Mkoa wa Dar es salaam Adolph Hallii akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Dar es salaam na kukupongeza chama cha AAT kwa kazi nzuri wanayofanya ya kutoa elimu mashuleni kuhusu matumizi sahihi ya alama za usalama barabarani.
Afisa Michezo wa Mkoa wa Dar es salaam Adolph Hallii akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Dar es salaam na kukipongeza chama cha AAT kwa kazi nzuri wanayofanya ya kutoa elimu mashuleni kuhusu matumizi sahihi ya alama za usalama barabarani.

Aidha chama cha (AAT) licha ya kuzindua awamu ya pili ya mradi wa kuelimisha wanafunzi juu ya matumizi sahihi ya alama za barabarani, pia kimezindua kampeni ya WEKA SIMU YAKO PEMBENI ambayo ina lengo kuwashawishi madereva kuweka simu zao pembeni na ikibidi kuzizima kabisa wakati wanaendesha vyombo vya moto.

668 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/04/05/neema-vyama-tumieni-michezo-kutoa-elimu-kwa-jamii/">
RSS