MAAZIMIO YA KAMATI YA KUSIMAMIA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA

Wajumbe wa kamati ya ngumi za kulipwa Tanzania wakiongozwa na mwenyekiti Mzee Emmanuel Saleh (kulia), Yahaya Poli- katibu (katikati) na Juma Ndambile - Mjumbe (kushoto) wakizungumza na waandishi wa Habari kuhusu maazimio ya kamati baada ya kukusanya maoni ya wadau wa Ngumi za kulipwa
Wajumbe wa kamati ya ngumi za kulipwa Tanzania wakiongozwa na mwenyekiti Mzee Emmanuel Saleh (kulia), Yahaya Poli- katibu (katikati) na Juma Ndambile – Mjumbe (kushoto) wakizungumza na waandishi wa Habari kuhusu maazimio ya kamati baada ya kukusanya maoni ya wadau wa Ngumi za kulipwa.

Kamati ya kusimamia ngumi za kulipwa nchini, inayoongozwa na mwenyekiti Mzee Emmanuel Saleh imeeleza maazimio yake baada ya kukusanya maoni  kutoka kwa wadau mbalimbali wa ngumi za kulipwa wakiwemo,  waamuzi, walimu, wakuzaji (mapromota), mabondia pamoja na mawakala,  maazimio hayo wameyatoa katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika tarehe 12 Aprili, 2018,  katika moja ya kumbi za uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Mheshimiwa Mwakyembe baada ya kuiteuwa  kamati hiyo mwanzoni mwa mwaka huu aliagiza kutekeleza yafuatayo:

  • Kuendelea kukusanya maoni ya wadau kuhusu Rasimu ya Katiba ya chombo cha kusimamia ngumi za kulipwa.
  • Kukutana na wadau wa ngumi za kulipwa kwa nyakati tofauti kujadili maendeleo ya mchezo wa ngumi za kulipwa Tanzania.

Moja  ya azimio la kamati hiyo baada ya kukutana na wadau ni utoaji wa leseni kwa wadau wa ngumi za kulipwa, ambapo kamati itatoa leseni kwa kila kada inayojihusisha na ngumi za kulipwa ili iweze kutambulika na gharama zake ni;

  • Bondia                                                                 12,000/=
  • Kocha                                                                   20,000/=
  • Promota                                                               50,000/=
  • Maofisa (waamuzi na watunza muda)           50,000/=

Aidha kamati imetoa muda wa majuma matatu kuanzia tarehe 12 April, 2018 hadi tarehe 31 April, 2018 kila mdau awe amepata leseni yake, hakuna mdau atakayeruhusiwa kujihusisha na ngumi za kulipwa kama hana leseni.

Pili ni usimamizi wa ngumi za kulipwa ambapo kamati imesisitiza kwamba Michezo yote ya ngumi za kulipwa nchini itasimamiwa na kamati na kama utaratibu unavyofahamika ulimwenguni kote mapambano ya kugombea mikanda huwa chini ya wenye mikanda.

Hata hivyo waandaaji wa mapambano ya ngumi za kulipwa wanalazimika kuomba kwa kamati kwa kuwasilisha nyaraka zote muhimu zinazohusiana na mpambano huo ikiwemo mikataba na hati za usajili, kamati imewasisitiza waandaaji pamoja na mabondia kuheshimu mikataba watakayoingia, kamati haitamfumbia macho yeyote ambaye atathibitika kukiuka mkataba husika, vilevile, mabondia toka nje ya nchi wanaokuja kucheza ni lazima wapewe vibali toka Baraza la Michezo.

Tatu ni utaratibu wa kusafiri nje ya nchi ambapo kamati imeazimia kwamba kuanzia tarehe 21 Machi, 2018 maombi yote yatalipiwa asilimia tano (5%) ya malipo ya bondia yaliyotajwa kwenye mkataba, vilevile maombi yanatakiwa kuwasilishwa kwa kamati mapema ili iweze kuyashughulikia na kuyawasilisha katika Baraza siku 14 kabla ya safari.

 

804 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/04/12/maazimio-ya-kamati-ya-kusimamia-ngumi-za-kulipwa-tanzania/">
RSS