SOPHIA VIGGO REIFFENSTEIN AIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI TLGU

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limesaidia kuratibu na kusimamia uchaguzi wa Chama cha Gofu cha Wanawake (TLGU) uliofanyika tarehe 21 Aprili 2018 kwenye Klabu ya Gofu Lugalo jijini Dar es Salaam.

Katika uchaguzi huo, Sophia Viggo Reiffenstein ndiye aliyepewa ridhaa na wapiga kura kukiongoza TLGU kama Rais kwa Awamu ya miaka miwili baada ya kupata kura 16 kati ya kura 18 zilizopigwa.

Anita James Siwale aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais kwa kupata kura 17 za ndiyo kutoka kwa wajumbe baada ya kuwa mgombea pekee katika nafasi hiyo, huku kwa upande wa nafasi ya Katibu Mkuu, Maria Alphonce Sebastian akiibuka kidedea kwa kupata kura 17 za ndiyo na kura 1 ya hapana baada ya kuwa mgombea pekee katika nafasi hiyo.

Aidha uongozi huo utadumu madarakani kwa kipindi cha miaka miwili (2) kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha Gofu cha Wanawake (TLGU).

Mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo Mwenyekiti na msimamizi Mkuu wa Uchaguzi huo kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Benson Chacha ameupongeza uongozi mpya na kuutaka uongozi huo Kufanya marekebisho ya katiba ya Chama ili iendane na wakati ndani ya miezi mitatu, Viongozi waliochaguliwa kukutana na BMT mapema ili waweze kupewa miongozo ya kutekeleza majukumu yao pamoja na viongozi kuapishwa, Kufanya uchaguzi wa kuziba nafasi ambazo hazikupata wagombea kama vile Katibu wa Mashindano na katibu wa Handcap, Kuandaa timu na kushiriki kwenye mashindano mbalimbali.

“Napenda kuupongeza sana uongozi mpya uliochaguliwa kuingia madarakani, ila tu niwaombe mbadilishe katiba ya Chama ili  iendane na wakati ndani ya miezi mitatu, Viongozi Mliochaguliwa mkutane na BMT mapema ili muweze kupewa miongozo ya kutekeleza majukumu yenu pamoja na  viongozi kuapishwa,” Alisema Chacha.

Nae Rais wa TLGU Sophia Viggo Reiffenstein ameushukuru uongozi wa BMT kwa kusimamia vyema uchaguzi huo na kuahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na Baraza sambamba na kuwataka viongozi waliochaguliwa kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kuwa shughuli za TLGU zinasimamiwa na kuendelezwa ipasavyo.

“Naushukuru sana Uongozi wa BMT kwa kusimamia vyema uchaguzi na Kuahidi kutekeleza maelekezo yote tuliyopewa na Baraza na niwaombe viongozi wote mliochaguliwa kufanya kazi kwa bidiii ili kuhakikisha kuwa shughuli za TLGU zinasimamiwa na kuendelezwa ipasavyo,”Alisema Sophia.

1,074 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/04/21/sophia-viggo-reiffenstein-aibuka-kidedea-uchaguzi-tlgu/">
RSS