KIGANJA: LIPIGANIENI TAIFA KIZALENDO MLETE MEDALI KUTOKA “ISFA”MOROCCO

Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja akizungumza mbele ya waandishi wa Habari Tarehe 1Mei, 2018 wakati wa kuaga timu ya wachezaji wa kuogelea inayokwenda nchini Morocco kushiriki katika mashindano ya kuogelea kwa shule mbalimbali Duniani ISFA
Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja akizungumza mbele ya waandishi wa Habari Tarehe 1Mei, 2018 wakati wa kuaga timu ya wachezaji wa kuogelea inayokwenda nchini Morocco kushiriki katika mashindano ya kuogelea kwa shule mbalimbali Duniani ISFA.

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa BMT Mohamed Kiganja ameitakata timu ya wachezaji 7 wa mchezo wa kuogelea inayoelekea jijini Marakech nchini Morroco katika mashindano ya kuogelea kwa wachezaji wanaosoma shule za Sekondari Duniani (ISF), kujituma ili kuweza kurejea nyumbani na ushindi.

Katibu Kiganja ameyasema hayo wakati akiiaga na kuikabidhi bendera timu hiyo leo hii tarehe 1 Mei, 2018, katika moja ya kumbi za uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam, ambapo amesisitiza kuwa ni vyema wachezaji hao wakajitume katika mashindano hayo ili waweze kufanya vizuri na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania.

Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja akikabidhi Bendera kwa Timu ya kuogelea inayokwenda kushiriki katika Mashindano ya kuogelea ya "ISFA"nchini Morocco.
Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja akikabidhi Bendera kwa Timu ya kuogelea inayokwenda kushiriki katika Mashindano ya kuogelea ya “ISFA”nchini Morocco.

“ni vyema nyinyi kama wachezaji kufanya bidii katika mashidano haya maana ndio mara yetu ya kwanza kuweza kushiriki kama nchi hivyo basi ni vyema mkaonyesha nidhamu ya hali juu nchini Morocco ili muweze kuipeperusha vyema  bendera yetu,” Alisema Kiganja.

Baadhi ya wachezaji wa kuogelea wanaokwenda nchini Morocco kushiriki katika mashindano ya Kuogelea ya ISFA
Baadhi ya wachezaji wa kuogelea wanaokwenda nchini Morocco kushiriki katika mashindano ya Kuogelea ya ISFA

Aidha Katibu Kiganja amevitaka vyama vya Michezo nchini kujitambua, ili kuweza kuhahakisha kunakuwa na wigo mpana katika Michezo mbalimbali, sanjari na viongozi kuwa weledi katika kazi zao na sio kutumia udikteta wa kuendelea kutaka kukaa madarakani ilhali wanachama wanataka mabadiliko na maendeleo.

“niombe utawala bora katika vyama vya Michezo hapa nchini, viongozi waache udikteta na uchu wa madaraka kutaka kuendelea kukaa madarakani muda mrefu jambo ambalo linadhohofisha maendeleo ya Michezo nchini,”Alisema Kiganja.

Kocha wa Timu ya Taifa ya mchezo wa kuogelea John Belela akizungumza na waandishi wa Habari leo 1Mei, 2018 wakati wa kuagwa kwa timu hiyo kuelekea Nchini Morocco katika mashindano ya kuogelea ya ISFA, na kuhaidi kuwa timu itafanya vizuri kwani wamefanya maandalizi ya kutosha na wachezaji kiujumla wapo vizuri kiafya.
Kocha wa Timu ya Taifa ya mchezo wa kuogelea John Belela akizungumza na waandishi wa Habari leo 1Mei, 2018 wakati wa kuagwa kwa timu hiyo kuelekea Nchini Morocco katika mashindano ya kuogelea ya ISFA, na kuhaidi kuwa timu itafanya vizuri kwani wamefanya maandalizi ya kutosha na wachezaji kiujumla wapo vizuri kiafya.

Kwa upande wake Kocha wa Timu ya Taifa ya kuongelea John Belela amesema anaamini wachezaji wake watafanya vizuri katika mashindano hayo kwani wamepata maandalizi ya kutosha na wapo vizuri kiafya hivyo kuna matumaini makubwa ya kuweza kufanya vizuri nchini Morocco.

Katibu Mkuu wa BMT katika mwenye shati la kitenge akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa mchezo wa kuogelea, wakiwemo viongozi wa Chama cha kuogelea na wazazi wa wachezaji wa kuogelea.
Katibu Mkuu wa BMT katika mwenye shati la kitenge akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa mchezo wa kuogelea, wakiwemo viongozi wa Chama cha kuogelea na wazazi wa wachezaji wa kuogelea.

“ninaamini kuwa tutafanya vizuri kwani tumejiandaa vizuri na wachezaji wangu wapo katika hali nzuri ya kiafya, hivyo tuna matumaini makubwa ya kufanya vizuri nchini Morocco,”Alisema Belela.

 

1,368 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by EmailO
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/05/01/kiganja-lipiganieni-taifa-kizalendo-mlete-medali-kutoka-isfamorocco/">
RSS