MHESHIMIWA MWAKYEMBE (Mb) AIPA TANO SERENGETI BOYS

Mheshimiwa Waziri Mwakyembe akiwakumbatia wachezaji wa Serengeti Boys baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakitokea nchini Burundi kushiriki michuano ya Cecafa U17 na kufanikiwa kutwaa kombe hilo.
Mheshimiwa Waziri Mwakyembe akiwalaki wachezaji wa Serengeti Boys baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakitokea nchini Burundi kushiriki michuano ya Cecafa U17 na kufanikiwa kutwaa kombe hilo.

Waziri wa Habari, utamaduni, sanaa na Michezo Mheshimiwa Harrison Mwakyembe(Mb)  amekipongeza kikosi cha timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys, kwa kutwaa ubingwa wa kombe la Cecafa baada ya kuiangamiza timu ya vijana ya Somalia kwa mabao mawili kwa bila katika mchezo wa fainali iliyochezwa uwanja wa Ngozi nchini Burundi.

Mheshimiwa Mwakyembe akiwa amelibeba kombe la ubingwa wa Cecafa U17, lililoletwa Nchini na Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys.
Mheshimiwa Mwakyembe akiwa amelibeba kombe la ubingwa wa Cecafa U17, lililoletwa Nchini na Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys.

Mheshimiwa Mwakyembe ametoa pongezi hizo baada ya kuipokea timu hiyo iliwayowasili kwa shirika la   Ndege ya “Rwanda airline” usiku wa kuamkia tarehe 1 Mei, 2018 katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam.

 

Timu ya Taifa ya vijana Serengeti Boys ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa Julius Kambarage Nyerere, wakitokea nchini Burundi waliposhiriki katika michuano ya Cecafa U17 na kufanikiwa kutwaa kombe hilo kwa kuifunga timu ya somalia kwa mabo 2-0 katika mchezo wa Fainali.
Timu ya Taifa ya vijana Serengeti Boys ikiwasili katika uwanja wa Ndege wa kimataifa Julius Kambarage Nyerere, wakitokea nchini Burundi waliposhiriki katika michuano ya Cecafa U17 na kufanikiwa kutwaa kombe hilo kwa kuifunga timu ya somalia kwa mabo 2-0 katika mchezo wa Fainali.

IMG_0365“niipongeze sana timu yetu ya vijana Serengeti Boys kwa kufanya vizuri kweli na kufanikiwa kutwaa ubingwa katika mashindano ya Cecafa U17 kule nchini Burundi, wameipeperusha vyema bendera ya Tanzania na kuonyesha uzalendo wa hali ya juu, kwa kweli tunajivunia timu hii,” Alisema Mheshimiwa Mwakyembe.

Aidha Mheshimiwa Mwakyembe amesema ushindi walioupata Serengeti boys sio wao peke yao bali ni wa Taifa zima na hii ni chachu tosha sasa kuelekea katika maandalizi ya mashindano ya kombe la mataifa barani afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka kumi na saba (U17) itakayofanyika hapa nchini mwakani 2019.

waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Harrison Mwakyembe (Mb) mwenye shati la kitenge watatu kutoka kuli mstari wa Nyuma akiwa katika picha ya pamoja na timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka kumi na saba, baada ya kuipokea timu hiyo katika uwanja wa Ndege wa kimataifa Julius Kambarage Nyerere ikitokea nchini Burundi kushiriki katika mashindano Cecafa U17 na kufanikiwa kutwaa ubingwa huo.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Harrison Mwakyembe (Mb) mwenye shati la kitenge watatu kutoka kulia mstari wa Nyuma akiwa katika picha ya pamoja na timu ya taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka kumi na saba, baada ya kuipokea timu hiyo katika uwanja wa Ndege wa kimataifa Julius Kambarage Nyerere ikitokea nchini Burundi kushiriki katika mashindano Cecafa U17 na kufanikiwa kutwaa ubingwa huo.

“vijana hawa bado ni wadogo sana, katika kikosi hiki hakuna mchezaji ata mmoja ambaye amezidi umri wa miaka 16, kwa hiyo hawa vijana tunawaandaa kwa ajili ya mashindano ya mwaka kesho wawe ndio u17 kweli, tunatakiwa tuwape mazoezi mengi ya kimataifa na nina uhakika mwakani kombe litabaki nchini Tanzania,”Alisema Mh. Mwakyembe.

Baadhi ya mashabiki kindakindaki nchini waliojitokeza kuwalaki Serengeti Boys katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere usiku wa kuamkia Mei Mosi 2018.
Baadhi ya mashabiki kindakindaki nchini waliojitokeza kuwalaki Serengeti Boys katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere usiku wa kuamkia Mei Mosi 2018.

Katika mashindano hayo Serengeti Boys ilitoka sare ya 1-1 na timu ya taifa ya Uganda, kabla ya kuifunga Sudan kwa mabao 6-0 na baadaye kuichapa Kenya kwa mabao 2-1 kwenye nusu fainali na kushinda mabao 2-0 dhidi ya Somalia kwenye mchezo wa Fainali.

138 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/05/01/mheshimiwa-mwakyembe-mb-aipa-tano-serengeti-boys/">
RSS