WAZIRI MWAKYEMBE AZINDUA BARAZA LA 14 LA BMT

Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dokta Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa Baraza la 14 la Michezo la Taifa tarehe 8 Mei, 2018.
Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dokta Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa Baraza la 14 la Michezo la Taifa tarehe 8 Mei, 2018.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Harrison Mwakyembe (Mb) amelitaka Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuleta mabadiliko makubwa katika tasnia ya maendeleo ya Michezo nchini kwa kuzingatia sheria ya Baraza ambayo ni sheria ya bunge Na.12 ya mwaka 1967 na marekebisho yake Namba 6 ya mwaka 1971.

Agizo hilo amelitoa tarehe 8 Mei, 2018 wakati akizindua Baraza hilo lenye wajumbe 10 aliloliteua tarehe 9 Februari 2018, katika moja ya kumbi za uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, ambapo pia Mheshimiwa Mwakyembe ameagiza kuanzishwa mfuko wa maendeleo ya Michezo nchini ambao utakuwa na vyanzo endelevu vya mapato na ili kufanikisha jambo hili lazima vyanzo vya mapato vya kisheria viboreshwe na vyanzo vipya vibuniwe na kuanzishwa ili kumudu majukumu mapana ya Baraza.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa BMT pamoja na wadau wa vyama mbalimbali vya michezo nchini.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa BMT pamoja na wadau wa vyama mbalimbali vya michezo nchini.

“Ni imani yangu kuwa tumefanya uteuzi wa wajumbe wa Baraza la Michezo kwa kuzingatia umakini na uwezo wao kwa kila mmoja tukiwa na malengo ya kuongeza ufanisi wa chombo hiki muhimu katika usimamizi wa maendeleo ya michezo nchini,hivyo basi muanzishe mfuko wa maendeleo ya Michezo ambao utakuwa na vyanzo endelevu vya mapato,” Alisema Mhe. Mwakyembe.

Aidha waziri Mwakyembe amesema Baraza lina wajibu wa kuendelea kufanya mapitio ya sheria iliyounda Baraza ili kuwa na Sheria inayoendana na hali halisi pamoja na matakwa ya maendeleo ya Michezo ya leo Tanzania na duniani kote, kuhakikisha wanafanya mikutano na wadau wa Michezo katika ngazi za mikoa na wilaya kubaini changamoto zao na kufuatilia maendeleo yao.

“niwaombe mtoe mafunzo ya utawala bora na namna nzuri ya kuongoza vyama na mashirikisho ya kitaifa ili kupunguza changamoto mbalimbali  ikiwemo migogoro isiyo ya lazima na kuleta ustawi katika kuendeleza Michezo nchini,hakikisheni kuwa vyama vya Michezo vinaheshimu katiba zao kwa kuheshimu vipindi vya uongozi na kufanya uchaguzi muda unapofika,”Alisema Mhe. Mwakyembe.

Mwenyekiti wa Baraza la 14 Leodgar chilla Tenga, akimshukuru Mheshimiwa waziri Mwakyembe kwa kuwaamini na kuwateua kwa lengo la kusimamia maendeleo ya Michezo nchini.
Mwenyekiti wa Baraza la 14 Leodgar chilla Tenga, akimshukuru Mheshimiwa waziri Mwakyembe kwa kuwaamini na kuwateua kwa lengo la kusimamia maendeleo ya Michezo nchini.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Baraza la kumi la nne Leodgar Tenga, amemshukuru Mheshimiwa waziri Mwakyembe kwa kuwaamini na kuwateua kwa lengo la kusimamia maendeleo ya Michezo nchini, na kuahidi kufanya tathmini ya hali halisi ya maendeleo ya Michezo, kutumia tathmini hiyo kutengeneza mpango mkakati wa kitaifa wa maendeleo ya Michezo nchini pamoja na kuhakikisha kuwa Michezo inaongozwa kwa kuzingatia msingi wa utawala bora.

“mheshimiwa Waziri tunakushukuru sana kwa kutuamini na kututeua kwa lengo la kusimamia maendeleo ya Michezo nchini na tunaahidi kufanya tathmini ya hali halisi ya maendeleo ya Michezo, kutumia tathmini hiyo kutengeneza mpango mkakati wa kitaifa wa maendeleo ya Michezo pamoja na kuhakikisha kuwa Michezo inaongozwa kwa kuzingatia msingi wa utawala bora,”Alisema Tenga.

54 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/05/08/waziri-mwakyembe-azindua-baraza-la-14-la-bmt/">
RSS