KAMATI MPYA ZA KUSIMAMIA NGUMI ZATANGAZWA TENA KUKAMILISHA MAJUKUMU YALIYOSALIA.

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja wakati akitangaza kamati za kusimamia ngumi za ridhaa na kulipwa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo hii katika moja ya ukumbi wa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja wakati akitangaza kamati za kusimamia ngumi za ridhaa na kulipwa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo hii katika moja ya ukumbi wa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja  kwa niaba ya Waziri mwenye dhamana ya michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ametangaza tena kamati itakayolisaidia baraza katika kusimamia ngumi za kulipwa, pamoja na kuiongezea muda kamati ya ngumi za ridhaa ili kamati hizo ziweze kukamilisha yale yaliyoelekezwa awali na kuwa na vyombo vitakavyosimamia ngumi hizo nchini, tukio lililofanyika leo tarehe 9 Mei, 2018 katika moja ya kumbi za uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kiganja alisema kuwa, tarehe 3 Januari, 2018, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Harrison Mwakyembe (Mb) aliteua wajumbe 13 kuunda kamati ya ngumi za kulipwa ambayo ingetengeneza Rasimu ya katiba ya chombo cha kusimamia ngumi za kulipwa nchini Tanzania, vivyo hivyo, tarehe 24  Februari, 2018 alisimamisha uchaguzi wa shirikisho la ngumi za ridhaa kwa kuwa katiba ya shirikisho ilikuwa na mapungufu na kutakiwa kufanyiwa maboresho.

Aliendelea kuwa, mambo muhimu ambayo kamati hizo zilitakiwa kuyatekeleza  ni pamoja na kuboresha katiba zao kwa kupokea maoni kutoka kwa wadau mbalimbali ili kuwa katiba bora zao, kuratibu mikutano ya kujadili rasimu za katiba hizo, na kuandaa mkutano mkuu wa uchaguzi ili wadau wa ngumi waweze kuwa na viongozi makini watakaosimamia ngumi za kulipwa na za ridhaa kupiga hatua kwa kuleta sifa kwa Taifa.

“Kamati hizi tulizielekeza kufanyia maboresho katiba zao kwa kuchukua maoni kutoka kwa wadau wao ili kuwa na katika bora zitakazopeleka ngumu katika hatua nzuri pamoja na kuandaa mkutano mkuu wa uchaguzi ili  kuwa viongozi makini wa kusimamia ngumi hizi,”alisisitiza Kiganja.

Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia ngumi za kulipwa Emmanuel Saleh (kushoto), Yahya Poli katibu (katikati) na Makamu mwenyekiti Joe Anea kulia
Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia ngumi za kulipwa Emmanuel Saleh (kushoto), Yahya Poli katibu (katikati) na Makamu mwenyekiti Joe Anea kulia.

Wajumbe waliotangazwa tena kwa upande wa ngumi za kulipwa ni  Emmanuel  Saleh  Mwenyekiti,Joe Anea Makamu Mwenyekiti,Yahya Poli katibu, Habib Kinyogoli Mjumbe,Dr. Killaga M.Killaga mjumbe na Fike Wilson Mjumbe.

Hata hivyo,  Mheshimiwa waziri ameamua kupunguza idadi ya wajumbe wa kamati na kubaki wajumbe 6 kutokana na majukumu ambayo ilipewa kusalia machache ambapo kamati aliyoiteuwa tena anaamini itaweza kuyakamilisha kikamilifu na kwa wakati.

Aidha, Mhe. Waziri, ameipongeza kamati yote ya ngumi za kulipwa kwa ujumla wake kwa umoja wao na kwa kazi kubwa waliyoifanya kwa faida ya Taifa na kwa muda mchache wa miezi 3.

Kwa upande wa Shirikisho la ngumi za ridhaa , Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa Mohamed Kiganja amewarudisha wajumbe wote wa kamati hiyo ila amewaongezea muda  na  kuwataka kufanya uchaguzi ifikapo Julai  7 mwaka huu, ambapo, aliwateua Februari 24 mwaka huu alipoahirisha uchaguzi wao na ulitakiwa kukoma tarehe 24 Mei, 2018.

Kamati ya shirikisho la ngumi za ridhaa wajumbe wake ni Muta Rwakatare -mwenyekiti, Samwel Sumwa Makamu – Mwenyekiti, Yono kevela- Mjumbe, Lukas Rutainurwa Mjumbe, Aisha Veneatus – Mjumbe, na Mohamed  A. Mohamed- Mjumbe.

Kamati hizi zitaendelea kulisaidia  na kulishauri Baraza la Michezo la Taifa kwa kuratibu shughuli za kila siku za ngumi za kulipwa na ridhaa nchini Tanzania na   zitaendelea kufanya kazi hizo kuanzia leo tarehe 10 Mei, 2018 baada ya kutangazwa tena rasmi.

1,449 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/05/10/kamati-mpya-za-kusimamia-ngumi-zatangazwa-tena-kukamilisha-majukumu-yaliyosalia/">
RSS