KIGANJA:WAJUMBE HAWAKUKOSEA KUMCHAGUA PROF. MTAMBO KUWA MAKAMU MWENYEKITI.

Katibu Mkuu wa baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja amesema kuwa, wajumbe wa Baraza hawakukosea kumchagua Profesa Mkumbukwa Madundo Angelo Mtambo kuwa Makamu Mwenyekiti wa Leodgar Chilla Tenga ameifanyia kazi tasnia ya michezo kwa muda mrefu.

Kiganja ameyasema hayo tarehe 16 Mei, 2018 wakati wa mkutano wake na Waandishi wa habari ulioandaliwa kwa ajili kumtangaza Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa la 14 lililozinduliwa Mei 8 na Waziri Mwakyembe, mkutano uliofanyika leo katika moja ya kumbi za uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

“Prof. Madundo Mtambo amekuwa kwenye tasnia hii na kuifanyia kazi kwa muda mrefu hivyo,  Wajumbe hawakukosea kumchagua kuwa Makamu Mwenyekiti niimani yangu ataitendea haki nafasi hii,”alisema, Kiganja nakuongeza kuwa;.

Baraza la 14 la Michezo la Taifa (BMT) chini ya Mwenyekiti wake Leodgar Chilla Tenga, limemchagua Profesa Mkumbukwa Madundo Angelo Mtambo kuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo, uchaguzi uliofanywa katika kikao Maalum kilichofanyika tarehe 14 Mei, 2018.

Uchaguzi huo umefanywa na wajumbe wa Baraza ikiwa ni matakwa ya Sheria ya Baraza katika nyongeza fungu la 3(2) kipengele cha katiba na utaratibu wa Baraza kifungu cha 3(3) inavyoelekeza, ikiwa ni moja ya maagizo ya Waziri mwenye dhamana ya Michezo Mheshimiwa Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) katika uzinduzi wa Baraza hilo uliofanyika tarehe 8 Mei, 2018 kuwa wajumbe watumie fursa waliopata kumchagua Makamu Mwenyekiti ili asipokuwepo Mwenyekiti wasijisikie kupwaya au kuyumba.

Licha ya kuwa Mjumbe na Makamu Mwenyekiti katika Baraza Profesa Mtambo ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO).

Aidha, kiganja alieleza kuwa, Prof. Madundo Mtambo ni mwanamichezo halisi katika Michezo mbalimbali kwani katika mchezo wa mpira wa miguu ameshawahi kuchezea timu ya ofisi ya waziri mkuu mjini Dodoma, chuo kikuu cha Sokoine na reli Mkoani Morogoro, vilevile ni mchezaji wa Michezo kama vile Chess, Bao, vishale, Pool table na mpira wa Meza.

Hata hivyo, amewahi kuwa na nyadhifa mbalimbali kama vile mjumbe wa kamati ya ufundi wa chama mpira wa miguu mkoani morogoro, meneja wa timu jumuishi ya Mkoa wa Morogoro na Mjumbe wa kamati ya rufaa ya TFF.

Vilevile ni Mjumbe wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), na ni mlezi wa kituo cha kukuza vipaji vya soka Mkoani Morogoro, ambapo miongoni mwa wachezaji ambao amewakuza ni pamoja na Shomari Kapombe, Mzamiri Yassin, Shiza Kichuya, Juma Abdul, Hassan Kessy, Ally Shomari na wengine wengi.

Prof. Madundo Mtambo ni mmoja wa wajumbe 10 wanaounda Baraza la Michezo la Taifa (BMT) lililoteuliwa na Mheshimiwa Mwakyembe Tarehe 9 Februari, 2018, pamoja na Mwenyekiti wao Leodgar Chilla Tenga na wajumbe ni Beatrese Singano,Kanali Mstaafu Juma Ikangaa, John Joseph Ndumbaro, Rehema Sefu Madenge na Salmin Kaniki.

 

 

 

100 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/05/16/kiganjawajumbe-hawakukosea-kumchagua-prof-mtambo-kuwa-makamu-mwenyekiti-2/">
RSS