WAZIRI MWAKYEMBE AMWAGIZA MSAJILI WA VYAMA VYA MICHEZO KUZIANDIKIA BARUA YA ONYO KAMPUNI YA TPBO NA PST.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dkt. Harrison Mwakyembe  amemwagiza Msajili wa vyama vya Michezo  Ibrahim Mkwawa kuziandikia barua ya onyo kampuni  zinazojishughulisha na ngumi za kulipwa  ikiwemo “ Tanzania Brofessional Boxing  Organization (TPBO)  na “Pugilistic Syndicate of Tanzania (PST)  kutokana na kuendesha  mchezo huo kwa ubabe, uonevu na vitendo vya jinai, kutoheshimu kamati aliyoieteua pamoja Serikali.

Hayo ameyasema tarehe 22 Mei, 2018 wakati wa mkutano wake na Waandishi wa habari, Kamati ya muda ya ngumi za kulipwa na baadhi ya wadau wa ngumi, mkutano uliokuwa na lengo la kutoa maelekezo kuhusu namna ya uendeshaji ya ngumi hizo kwa kufuata taratibu zilizopo kisheria na za kamati aliyoiteuwa kusimamia mchezo huo.

Waziri alieleza kuwa, Mwenyekiti wa Kamati Mzee Emanuel Salehe amesema kuwa mchezo wa ngumi umegubikwa na vurugu lakini siyo vurugu bali ubabe, uonevu, na vitendo vya jinai  kwa  kuwa baadhi ya wanamasubwi  wamekuwa wakikamatwa  nje ya nchi kwa kuwa makontena yao ya dawa za kulevya na kupelekea wanamasubwi kuonewa pamoja na kuumia kwa kutokujua stahili zao kwa muda mrefu kwa kukosa uelewa.

Aliendelea kuwa, katika vurugu na fujo hizi kuna watu wamefaidika sana na kuna wanamasubwi wameumia  sana kwa kutokujua stahili zao katika mapambano mengi ya nje kwa kulipwa masilahi duni kupita kiasi na kueleza kuwa hili haliwezi kuendelea na ndio lengo la kuunda chombo cha muda cha kusimamia ngumi hizo  ili mikataba iwe wazi panapokuwa na mapambano ndani na nje ya nchi na mwanamasumbwi kulipwa pesa zake kabla ya pambano.

“Baadhi ya Wanamasubwi wamelipishwa pesa nyingi sana kwa kukosa uelewa wa hiyo mikataba na ndio lengo la kuunda chombo hiki ili mikataba iwe wazi kabla ya pambano,”alieleza Waziri na kuongeza kuwa:

“Naapa kuisafisha tasnia ya ngumi za kulipwa, na mwaagiza Msajili kuwaandikia barua ya onyo la mwisho kampuni ya TPBO na PST ambao ndio vinara wa vurugu na uonevu na sitasita kuwafungia wasipojirekebisha.”

Pia, Dkt. Mwakyembe amemwaagiza Msajili kuziandikia asasi zote za Kimataifa zinazotunza rekodi za mabondia na kuwaeleza kuhusu chombo husika cha kutuma rekodi za masumbwi  wa Tanzania na siyo hao walioichafua Kamati aliyoiteuwa yeye na kuiwasilisha taarifa hiyo mapema wiki hii.

Aidha, ameeleza kuwa, ataongea na Mkurugenzi Mkuu wa Uhamiaji kuwa hakuna Mwanamasumbwi yeyote kuruhusiwa kusafiri nje ya nchi bila kuwa na kibali kutoka BMT na Baraza hakuna kutoa kibali bila kupokea ushauri kutoka kwa kamati ya muda ya kusimamia ngumi za kulipwa aliyoiteua mwanzoni mwa mwaka huo, vilevile amewataka polisi kutoruhusu pambano lolote ambalo halina kibali kutoka Baraza la Michezo la Taifa.

Mhe. Mwakyembe ameahidi kufanya mkutano  na wadau wote wa masumbwi Tanzania mapema mwezi june wakiwemo wa Mikoani ili kuisafisha tasnia hii ambapo, tarehe watafahamishwa baadaye.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati iliyoteuliwa na Dkt. Mwakyembe Mzee Emanuel Saleh amesema kuwa, walipata ushirikiano wakutosha ingawa mwishoni wamepata changamoto  lakini ameahidi kuikamilisha kwa weledi katiba hiyo na wanaendelea  kupotea maoni mengine ambayo watayaweka kwenye kanuni za katiba ya chombo cha kusimamia ngumi za kulipwa nchini.

Mwenyekiti wa kamati ya muda ya ngumi za kulipwa Mzee Emanuel Saleh (kulia) akisema jambo kwa waandishi na wadau wa ngumi kabla ya Waziri Mwakyembe, kushoto ni Waziri.
Mwenyekiti wa kamati ya muda ya ngumi za kulipwa Mzee Emanuel Saleh (kulia) akisema jambo kwa waandishi na wadau wa ngumi kabla ya Waziri Mwakyembe (katikati), kushoto ni Mkurugenzi wa Michezo Yusuph Singo.

Katika hatua nyingine Msajili wa vyama vya Michezo Ibrahim Sapi Mkwawa alieleza kuwa, amefanya kazi na kamati kwa karibu na wamekamilika kwa asilimia nyingi pamoja na changamoto walizopitia,  na amemuahidi Waziri kuyafanyia kazi maagizo yake kwa wakati.

 

 

 

 

233 total views, 3 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by EmailO
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/05/22/waziri-mwakyembe-amwagiza-msajili-wa-vyama-vya-michezo-kuziandikia-barua-ya-onyo-kampuni-ya-tpbo-na-pst/">
RSS