WAZIRI MWAKYEMBE AAHIDI KUWAUNGA MKONO JICA KUINUA VIPAJI VYA WASICHANA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameahidi kufanya kazi na Taasisi ya Kimataifa ya Japan (JICA) kuendelea kuinua vipaji vya wasichana katika michezo mbalimbali ukiwemo wa riadha ambao wameanza nao.

Waziri Mwakyembe watatu kushoto akiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Japan (JICA) baada ya kumaliza kikao nao Mei 22,2018 chenye lengo la kuinua vipaji vya watoto wa kike kimichezo, kikao kilichofanyika katika Ofisi yake iliyopo jengo la Kimataifa la Mwl. Nyerere jijini Dar es salaam.
Waziri Mwakyembe watatu kushoto akiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka Taasisi ya Kimataifa ya Japan (JICA) baada ya kumaliza kikao nao Mei 22,2018 chenye lengo la kuinua vipaji vya watoto wa kike kimichezo, kikao kilichofanyika katika Ofisi yake iliyopo jengo la Kimataifa la Mwl. Nyerere jijini Dar es salaam.

Mhe. Mwakyembe ameyasema hayo jana tarehe 22 Mei, 2018 katika kikao alichofanya na baadhi ya viongozi kutoka katika taasisi hiyo ya kimataifa katika Ofisi zake zilizoko katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere uliopo jijini Dar es salaam.

Akiongea katika kikao hicho, Mwakilishi Mkuu wa Taasisi hiyo Toshio Nagase alisema, JICA wamejipanga kuendeleza urafiki wake na Tanzania katika nyaja tofauti ikiwemo ya Michezo ambapo, Novemba  24 hadi 25 mwaka huu watafanya shindano la riadha kwa wasichana kama walilofanya mwaka jana.

Nagase aliongeza kuwa, vilevile Octoba mwaka huu timu ya Watanzania 15 waliohusika kwa namna moja au nyingine kufanikisha mashindano ya riadha ya mwaka jana wakiwemo wachezaji na viongozi watasafiri kwenda nchini Tokyo Japan katika mji wa Nagai ambao ndio mji watakaofikia Watanzania katika mashindano ya Olympiki ya 2020, ambapo, watatembelea shule tofauti kujifunza Michezo mbalimbali na kuimarisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizi mbili.

Katika shindano la Novemba Dkt. Mwakyembe amesema kuwa atafanya kila linalowezekana kutafuta wadhamini wengine watakaosaidiana na taasisi ya JICA kufanikisha mashindano hayo yaweze kufana zaidi na  kulisemea bungeni wiki ijayo, pamoja na kumwomba “First Lady Mama Janeth Magufuli kuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo yenye kauli mbiu ya mwanamke kwanza “Ladies First Event” for 2018.

Kwa upande wake Balozi wa hiari wa JICA nchini Tanzania na Mjumbe wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Juma Ikangaa alisema kuwa, ameshauri wadhamini na kuwaendeleza wasichana katika mchezo huo kwa kuwa ndio mchezo ulioleta medali ya kwanza Tanzania katika mashindano ya Jumuiya ya Madola yaliyofanyika Congo Brazaville mwaka 1965 na mwanamama Theresia Dismas.

Lakini pia, Ikangaa alishauri Serikali kuimarisha Michezo ya “UMISSETA na UMITASHUMTA” kwa kuwa ndio inayoibua vipaji vya wachezaji wengi kwani hata yeye na wengine walipata sifa kwa nchi walitokea huko.

 

10 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/05/23/waziri-mwakyembe-aahidi-kuwaunga-mkono-jica-kuinua-vipaji-vya-wasichana/">
RSS