UONGOZI WA BFT ULIOMALIZA MUDA WAKE WAKABIDHI OFISI NA VIFAA KWA KAMATI ILIYOTEULIWA KUSIMAMIA NGUMI HIZO.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mchezo wa Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) Makore Mashaga akikabidhi karatasi iliyoandikwa vitu alivyokabidhi kwa Katabu wa Kamati iliyoteuliwa kusimamia ngumi hizo Mohamed Abubakar baada ya kusitishwa kwa uchaguzi Februari, 2018 kupisha marekebisho ya Katiba

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la ngumi za ridhaa Tanzania (BFT) Makore Mashaga amekabidhi Ofisi na vifaa vya Shirikisho hilo kwa Kamati ya muda iliyoteuliwa na aliyekuwa Katibu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Mohamed Kiganja baada ya kusitisha uchaguzi uliokuwa ufanyike Februari 24 mwaka huu mjini Dodoma na kuwataka wafanye marekebisho ya Katiba.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za shirikisho hilo zilizopo katika majengo ya zamani ya Baraza la Michezo la Taifa, tukio lililofanyika leo tarehe 30 Mei, 2018 jijini Dar es salaam.

Baadhi ya vilivyokabidhiwa ni pamoja akaunti ya benki, sanduku la posta, vyumba vitatu vya Ofisi walivyokuwa wakivitumia viongozi walimaliza muda wao na vifaa vikiwemo kabati 4, meza 3, Komputa, printa, mihuri, na nyaraka tofauti zikiwemo paspoti.

Baadhi ya vifaa vinavyoonekana ndivyo vilivyokabidhiwa kwa Kamati ya ngumi za Ridhaa
Baadhi ya vifaa vinavyoonekana ndivyo vilivyokabidhiwa kwa Kamati ya ngumi za Ridhaa

Mashaga alieleza kuwa, ataendelea kutoa ushirikiano kwa kamati iliyoteuliwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa BMT Mohamed Kiganja kwa sababu anapenda maendeleo ya ngumi na anaupenda mchezo huo.

“Nitaendelea kutoa ushirikiano kwa kamati kwakuwa napenda maendeleo ya ngumi nchini na naupenda mchezo huu,”alisema Mashaga.

Kwa upande wake Katibu wa Kamati ya muda iliyoteuliwa kusimamia ngumi za ridhaa Mohamed Abubakari alieleza kuwa, wataendelea kushirikiana na viongozi waliomaliza muda wao.

526 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/05/30/uongozi-wa-bft-uliomaliza-muda-wake-wakabidhi-ofisi-na-vifaa-kwa-kamati-iliyoteuliwa-kusimamia-ngumi-hizo/">
RSS