HATUTAKI MAMLUKI UMISSETA 2018.

Serikali kupitia wizara ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imesema haitafumbia macho wala kupepesa masikio kwa mikoa na viongozi wake watakaobainika kuwachezesha wachezaji mamluki katika mashindano ya UMISSETA 2018 jijini Mwanza.

Mwenyekiti wa michezo ya UMMISETA na UMITASHUMTA Taifa toka TAMISEMI Leonard Thadeo akizungumzia kuhusu mikoa itakayobainika kuwatumia wachezaji mamluki kufukuzwa pamoja na viongozi wake sanjari na kusimamishwa kushiriki kwa kipindi cha miaka mitano.
Mwenyekiti wa michezo ya UMMISETA na UMITASHUMTA Taifa toka TAMISEMI Leonard Thadeo akizungumzia kuhusu mikoa itakayobainika kuwatumia wachezaji mamluki kufukuzwa pamoja na viongozi wake sanjari na kusimamishwa kushiriki kwa kipindi cha miaka mitano.

Akizungumza wakati wa ufunguzi mdogo wa mashindano hayo, mwenyekiti wa michezo hiyo Taifa toka TAMISEMI Leonard Thadeo amesema mikoa itakayobainika kuwatumia wachezaji mamluki itafukuzwa pamoja na viongozi wake sanjari na kusimamishwa kushiriki kwa kipindi cha miaka mitano.

Aidha mwenyekiti huyo ameongeza kuwa hawatakuwa tayari kusimamisha ratiba au kukwamisha michezo hiyo ambayo imechukua muda na gharama kubwa kuandaa lakini pia ni lazima taratibu na kanuni zizingatiwe.

“hatutawavumilia mamluki katika michezo hii, mkoa utakaobainika utafukuzwa pamoja na viongozi wake wakiwamo mwenyekiti, meneja na kocha,” alisema Thadeo.

 

 

Katibu wa zamani wa Baraza la Michezo la Taifa BMT ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa maadhimisho ya Kitaifa Tanzania toka Ofisi ya Waziri Mkuu Mohammed S. Kiganja akizungumzia na kutilia mkazo suala la utovu wa nidhamu kwa wanafunzi waliopo kambini chuo cha ualimu Butimba sanjari na kugusia kauli mbiu ya mwaka huu "Michezo, Sanaa na Taaluma ni msingi wa maendeleo ya Mwanafunzi kwa Taifa letu"
Katibu wa zamani wa Baraza la Michezo la Taifa BMT ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa maadhimisho ya Kitaifa Tanzania toka Ofisi ya Waziri Mkuu Mohammed S. Kiganja akizungumzia na kutilia mkazo suala la utovu wa nidhamu kwa wanafunzi waliopo kambini chuo cha ualimu Butimba sanjari na kugusia kauli mbiu ya mwaka huu “Michezo, Sanaa na Taaluma ni msingi wa maendeleo ya Mwanafunzi kwa Taifa letu”
Katibu wa UMISSETA TAIFA 2018, Aaron Sokoni akizungumzia  jumla ya washiriki mwaka huu kuwa ni elfu tatu mia nane na tisini na mbili (3892), ikiwa wachezaji ni elfu tatu mia tatu na sitini( 3360) na viongozi ni mia Tano thelathini na mbili (532).
Katibu wa UMISSETA TAIFA 2018, Aaron Sokoni akizungumzia jumla ya washiriki mwaka huu kuwa ni elfu tatu mia nane na tisini na mbili (3892), ikiwa wachezaji ni elfu tatu mia tatu na sitini( 3360) na viongozi ni mia Tano thelathini na mbili (532).

Nae katibu wa UMISSETA TAIFA 2018, Aaron Sokoni amesema kuwa jumla ya washiriki mwaka huu ni elfu tatu mia nane na tisini na mbili (3892), ikiwa wachezaji ni elfu tatu mia tatu na sitini( 3360) na viongozi ni mia Tano thelathini na mbili (532).

IMG_0258“Tumefungua mashindano ila ufunguzi rasmi utafanyika tarehe 9 Juni, 2018 katika uwanja wa ccm kirumba jijini Mwanza,” alisema Sokoni.

79 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/06/04/hatutaki-mamluki-umisseta-2018/">
RSS