TIMU YA MWANZA NETIBOLI WANAWAKE WAANZA KWA KISHINDO UMISSETA 2018

Mashindano ya Umoja wa Michezo Shule za Sekondari Tanzania (UMISSETA) 2018, yameanza kutimua vumbi leo hii 4 Juni, 2018, katika vituo viwili vya chuo cha ualimu Butimba na Nsumba Sekondari jijini Mwanza.

Timu ya Mkoa wa Rukwa ikiliandama goli la Timu ya Mwanza katika kipindi cha pili baada ya kwenda mapunziko wakiwa nyuma magoli 23 kwa 6
Timu ya Mkoa wa Rukwa ikiliandama goli la Timu ya Mwanza katika kipindi cha pili baada ya kwenda mapunziko wakiwa nyuma magoli 23 kwa 6

Timu ya mkoa wa Mwanza netiboli wanawake wameanza kwa kishindo katika mashindano hayo baada ya kuifunga timu ya wanawake wa mkoa wa Rukwa kwa magoli 50 kwa 10 mchezo uliopigwa katika uwanja wa Nganza jijini Mwanza.

Timu ya Mkoa wa Mwanza ikifunga moja kati ya magoli yake iliyopata katika mchezo wake dhidi ya Rukwa.
Timu ya Mkoa wa Mwanza ikifunga moja kati ya magoli yake iliyopata katika mchezo wake dhidi ya Rukwa, pembeni ni mashabiki kindakindaki waliojitokeza kushuhudia mchezo huo.

IMG_0559

Katika michezo mingine ya mchezo huo iliyopigwa katika viwanja tofauti vya vituo hivyo timu ya mkoa wa Tabora wanawake iliweza kuichapa Timu ya Arusha kwa magoli 27 kwa 18, huku timu ya mkoa wa Katavi ikiichapa timu ya Pwani kwa magoli 24 kwa 17.

341 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/06/04/timu-ya-mwanza-netiboli-wanawake-waanza-kwa-kishindo-umisseta-2018/">
RSS