DAR ES SALAAM YAANZA KUNG’ARA UMISSETA 2018

Timu ya wavulana ya mpira wa miguu mkoa wa Dar e s saalam imeanza vyema mashindano ya UMISSETA 2018, kwa kufanikiwa kuichapa timu ya mkoa wa Lindi kwa mabao 2-0, mabao yaliyopatikana mwishoni kipindi cha kwanza na mwishoni kipindi cha pili cha mchezo.

Timu ya Mkoa wa Dar es salaam ikifunga goli lake la kwanza katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Mkoa wa Lindi uliopigwa katika uwanja wa shule ya msingi Butimba Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza.
Timu ya Mkoa wa Dar es salaam ikifunga goli lake la kwanza katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Mkoa wa Lindi uliopigwa katika uwanja wa shule ya msingi Butimba Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza.

Timu hiyo imepangwa katika kundi A na timu za mkoa wa Geita, Kigoma, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya na Ruvuma ambapo mpaka sasa timu ya mkoa wa Mbeya ndio inaongoza kundi hilo baada ya kujikusanyia jumla ya alama sita baada ya kuzifunga timu ya mkoa wa Lindi kwa bao 1-0 na timu ya mkoa wa Ruvuma kwa magoli 2-0.

Mchezaji wa Timu ya Mkoa wa Dar es salaam Chris Aweda akiongoza akiongoza mashambulizi kuelekea katika goli la Lindi, Mchezo wa kwanza ambao Dar es salaam aliweza kuibuka mshindi kwa kuifunga Lindi kwa magoli 2-0.

Kwa upande wa matokeo mengine timu ya Mkoa wa Lindi iliweza kuitungua Kigoma kwa magoli 4-1 katika mchezo wake wa kwanza,Geita wakaifunga timu ya Ruvuma kwa magoli 3-1 na kuifunga tena Kilimanjaro kwa goli 1-0.

Vijana wa Timu ya Dar es salaam wakishangilia moja ya magoli yao waliyofunga katika mchezo wao dhidi ya mkoa wa Lindi.
Vijana wa Timu ya Dar es salaam wakishangilia moja ya magoli yao waliyofunga katika mchezo wao dhidi ya mkoa wa Lindi.

Katika kundi B watoto wa makao makuu timu ya mkoa wa Dodoma imefanikiwa kuifunga timu ya Mkoa wa Simiyu kwa magoli 3-1, huku Pemba wakiifunga Songwe ambao ndio mabingwa watetezi kwa goli 1-0, sanjari na kuifunga Shinyanga kwa Goli 1-0.

Timu ya Mkoa wa Dar es salaam ikipasha misuli moto kabla ya kuingia katika mchezo wao dhidi ya mkoa wa Lindi.
Timu ya Mkoa wa Dar es salaam ikipasha misuli moto kabla ya kuingia katika mchezo wao dhidi ya mkoa wa Lindi.

Katika kundi C mkoa wa Arusha ulifanikiwa kuifunga timu ya Katavi kwa goli 2-1, huku katika kundi D Morogoro wakitoa suluhu na Manyara kwa kufungana mabao 1-1, Mara pia wakitoa Suluhu ya bila kufungana na timu ya Njombe, wakati Mtwara wakikubali kichapo cha goli 2-1 kutoka kwa timu ya mkoa wa Unguja na Njombe wakiifunga Kagera kwa goli 1-0.

32 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/06/05/dar-es-salaam-yaanza-kungara-umisseta-2018/">
RSS