WAZIRI MWAKYEMBE AUWAGIZA UONGOZI WA TSA KUANDAA TAARIFA YA UTEKELEZAJI YA KIPINDI CHAKE MADARAKANI.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Dr. Harrison Mwakyembe ameuagiza Uongozi wa Chama cha Mchezo  wa Kuogelea Tanzania (TSA) kuandaa taarifa ya utekelezaji katika kipindi walichokaa madarakani  kwa kushirikiano na viongozi waliojiuzulu ambao wengine wapo katika kamati ya muda  ambapo, taarifa hiyo wataiwasilisha katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi ambao Baraza la Michezo la Taifa limetakiwa kuuratibu mapema mwezi huu.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt. Harrison G Mwakyembe (katikati) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa pamoja 10 Juni, 2018, baina ya Serikali na viongozi wa zamani wa chama cha kuogelea nchini (TSA) kulia ni katibu Mkuu wa wizara, Susan Mlawi na Kushoto ni Kaimu katibu Mkuu wa BMT. Alex Nkenyenge.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt. Harrison G Mwakyembe (katikati) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa pamoja 10 Juni, 2018, baina ya Serikali na viongozi wa zamani wa chama cha kuogelea nchini (TSA) kulia ni katibu Mkuu wa wizara, Susan Mlawi na Kushoto ni Kaimu katibu Mkuu wa BMT. Alex Nkenyenge.

Hayo ameyasema tarehe 10 June, 2018 katika Mkutano wake aliouitisha kati yake  BMT na viongozi wa TSA pamoja Kamati ya muda iliyoteuliwa na Mkutano wa Wanachama  wa mchezo huo uliofanyika Februari 23 mwaka huu wakati wa mashindano ya Taifa yaliyofanyika Dare es salaam, mkutano uliofanyika jana katika Ukumbi wa habari Maelezo ulipo katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Dr. Mwakyembe wamewataka viongozi  hao pia, kuwasilisha taarifa zilizopo kisheria ikiwemo taarifa ya  mahesabu waliyotakiwa kuileta kwa Msajili wa vyama vya Michezo tangu mwezi Octoba mwaka jana lakini hawakufa hivyo,  ambapo amewataka kuiandaa na kuiwasilisha kwa Msajili mapema iwezekanavyo.

“Nauagiza uongozi wa TSA kuandaa taarifa ya utekelezaji  ya kipindi chote walichokuwepo madarakani  pamoja taarifa zilizopo kisheria ikiwemo ya mahesabu, iandaeni mapema na kuiwasilisha kwa Msajili,”alisisitiza Waziri Mwakyembe.

Hata hivyo, amelielekeza Baraza la Michezo la Taifa kusimamia shughuli zote za  chama hicho kwa kipindi hiki na kuratibu maandalizi ya uchaguzi ndani ya mwezi  mmoja ili hatimaye mchezo wa kuogelea uweze kuwa na viongozi makini watakaoupeleka katika hatua nzuri ya kimaendeleo.

Lakini pia, Dr. Mwakyembe amewaagiza Viongozi wa BMT akiwemo Kaimu Katibu Mkuu Alex Nkenyenge na Msajili Ibrahim Mkwawa pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Yusuph Singo kufanya kikao na Uongozi wa TSA na Kamati ya muda iliyomaliza muda wake na kuwasilisha Rasimu ya Katiba BMT tarehe 08 June, 2018 ili kuipitia Rasimu hiyo kipengele kwa kipengele ikiwemo suala la muungano Jumatano ya tarehe ya 13 wiki hii ili iweze kuwasilishwa kwake na hatimaye kwa Wanachama katika Mkutano Mkuu wa uchaguzi.

“Kaeni na Katibu wa BMT, Msajili, na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo mpitie kipengele kwa kipengele yakiwemo masuala ya Muungano tupate Katiba bora itakayopeleka mchezo huu pazuri, nataka chama kipya cha kuogelea,”alisema Dr. Mwakyembe.

Waziri alieleza kuwa, kati ya vyama ambavyo havijikaa sawa ni pamoja na chama cha kuogelea, lakini ameahidi kuwa, atahakikisha amemaliza sintofahamu iliyopo katika baadhi ya vyama vya Michezo na amekutana na baadhi ya vyama na kuahidi kukutana na vyama vyote ifikapo mwisho wa mwaka huu na kuondoa migogoro yaliyopo katika Michezo ikiwemo viongozi kujimilikishia vyama.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa BMT Alex Nkenyenge amemwahidi Mhe. Waziri kuyatekeleza yote aliyoagiza na kuendelea na  maandalizi ya kuelekea kwenye uchaguzi.

Katika hatua nyingine viongozi wa TSA na wale wa Kamati ya muda wamemuahidi Waziri kushirikiana na BMT kukamilisha Katiba ili kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara Bi. Susan Mlawi, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Yusuph Singo, Viongozi wa BMT, Viongozi wa TSA akiwemo, Mwenyekiti Alex Moshi, Katibu Mkuu Ramadhan Namkoveka, Mwekahazina msaidizi  Ayoub Andrew, Wajumbe ni Abdulwahab Mohamed, Mwadin Haji,  na kutoka katika Kamati ya muda na baadhi yao waliojiuzuli ni Mwenyekiti Alexander Mwaipai, Imani Ahmaya, Amina Mfaume,Inviolata Itatiro na Anna Shanalingigwa.

 

 

86 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by EmailO
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/06/11/waziri-mwakyembe-auwagiza-uongozi-wa-tsa-kuandaa-taarifa-ya-utekelezaji-ya-kipindi-chake-madarakani/">
RSS