NKENYENGE: NAOMBA USHIRIKIANO WA WADAU ILI TUFANIKIWE KATIKA MICHEZO NCHINI

Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Alex Nkenyenge ameeleza kuwa, anaomba ushirikiano wa wadau wote wa michezo wakiwemo viongozi wa michezo, wanamichezo, Kamati za Michezo za Mikoa na Halmashauri zilizopo chini ya Makatibu Tawala kutekeleleza wajibu wao katika michezo kadri sheria inavyowataka  ili kuweza kufanikiwa katika Michezo nchini kwakuwa Michezo inachezwa katika ngazi zote.

Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Alex Nkenyenge akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushirikiano wa wadau wote wa michezo wakiwemo viongozi wa michezo, wanamichezo, Kamati za Michezo za Mikoa na Halmashauri zilizopo chini ya Makatibu Tawala kutekeleleza wajibu wao katika michezo kadri sheria inavyowataka  ili kuweza kufanikiwa katika Michezo nchini kwakuwa Michezo inachezwa katika ngazi zote.
Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Alex Nkenyenge akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushirikiano wa wadau wote wa michezo wakiwemo viongozi wa michezo, wanamichezo, Kamati za Michezo za Mikoa na Halmashauri zilizopo chini ya Makatibu Tawala kutekeleleza wajibu wao katika michezo kadri sheria inavyowataka ili kuweza kufanikiwa katika Michezo nchini kwakuwa Michezo inachezwa katika ngazi zote.

Hayo ameyasema mapema alipoingia katika Ofisi ya Baraza la Michezo la Taifa  baada ya kuteuliwa na Waziri Mwakyembe,  alipoulizwa na moja ya waandishi  ana mipango gani baada kuingia BMT ili kuona Michezo inafika katika hatua nzuri, tukio lililofanyika tarehe 12 Juni, 2018 katika Ofisi za BMT zilizopo uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

“Ninachoomba ni ushirikiano wa wadau wa Michezo Wakiwemo viongozi wa michezo, Wanamichezo na Kamati za Michezo za Mikoa na Halmashauri zilizopo chini Makatibu Tawala wa Mikoa, wote tukifanya kazi kwa ushirikiano Michezo itafika mahali pazuri na tukasonga mbele,”alisema Nkenyenge.

“Michezo inachezwa sehemu zote nani mali ya wananchi na inachezwa katika ngazi zote, baraza makao makuu yake yako Dar es salaam na wako watendaji sehemu mbalimbali hivyo tukishirikiana tunaweza kusonga mbele,”alisema Nkenyenge na kuongeza kuwa;

Katika kutekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na Bodi pamoja na menejimenti ya  baraza watatekeleza kwa mujibu wa  sheria na kanuni za bunge zilizoliunda BMT, ambapo alisema wameandaa programu  ya kufanya tathmini ya kile kilichofanyika kipindi kilichopita na kujipanga kwa mwaka unaofuata. Katika tathmini hiyo wamejipanga kukutana na wadau wa Michezo na makundi mbalimbali ili kuweza kujua uimara na mapungufu yaliyopo katika taasisi ili kujipanga kufanya vizuri zaidi.

Aidha katibu Nkenyenge amesema Baraza limeandaa program maalum kwa ajili ya kufanya tathmini ili kujuwa ni kitu gani ambacho Baraza linafanya na taswira ikoje kwa jamii ya Tanzania kuhusu Baraza, je mapungufu ni yapi na mazuri ni yapi ili kuhakikisha linasimama imara na Michezo inapiga hatua kubwa zaidi nchini.

 

32 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/06/12/nkenyenge-naomba-ushirikiano-wa-wadau-ili-tufanikiwe-katika-michezo-nchini/">
RSS