MKURUGENZI WA MAENDELEO YA MICHEZO AWATAKA VIONGOZI WA TSA KUTORUDI NYUMA WASIMAMIE MAAGIZO YA WAZIRI.

Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo Yusuph singo (tisheti ya bluu kushoto) Kaimu Katibu Mkuu wa BMT (mwenye tai) wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mapitio ya rasimu ya katiba ya TSA tarehe 13 Juni, 2018 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo Yusuph singo (tisheti ya bluu kushoto) Kaimu Katibu Mkuu wa BMT (mwenye tai) wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mapitio ya rasimu ya katiba ya TSA tarehe 13 Juni, 2018 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa maendeleo ya Michezo Yusuph Singo amewataka viongozi wa mchezo wa kuogelea nchini (TSA) kutorudi nyuma katika malumbano badala yake wasimamie maelekezo ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo  Mhe. Mwakyembe ya kuiboresha katiba ya chama chao na hatimaye waelekea katika uchaguzi wao mkuu ulioelekezwa kufanyika mapema baada ya kukamilika kwa katiba.

Maelezo hayo ameyatoa wakati wa kikao cha kuipitia katiba ya chama cha mchezo wa kuogelea nchini  baada ya kuagizwa kufanya hivyo na Mhe. Waziri mwishoni mwa wiki katika kikao chake na viongozi wa mchezo huo tarehe 10 Juni, 2018, kikao kilichofanyika jana tarehe 13 June, 2018 katika moja ya kumbi za uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

 

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Yusuph Singo (kulia) akitoa maelekezo kwa wajumbe wakati wa mapitio ya rasimu ya katiba ya TSA kushoto kwake ni Kaimu Katibu Mkuu wa BMT Alex Nkenyenge akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Yusuph Singo (kulia) akitoa maelekezo kwa wajumbe wakati wa mapitio ya rasimu ya katiba ya TSA kushoto kwake ni Kaimu Katibu Mkuu wa BMT Alex Nkenyenge akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi.

“Tusirudi nyuma tulikotoka kwenye malumbano,  tumepewa maelekezo na Waziri, lengo ni kuiboresha katiba hii itakayotusaidia sisi wote,”alisema Singo.

Rasimu hiyo ya Katiba ya chama cha kuogelea Tanzania imepitiwa kipengele kimoja baada kingine na wataalam wa Michezo akiwemo Mkurugenzi huyo wa Michezo Yusuph Singo,Kaimu  Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Alex Nkenyenge, Kaimu Msajili Ibrahim Mkwawa kwa pamoja na aliyekuwa Katibu wa TSA Ramadhan Namkoveka na wajumbe wote wa kamati ya muda iliyoundwa kuandaa rasimu hiyo akiwemo, Mwenyekiti Alexander Mwaipai, Imani Ahmaya, Amina Mfaume,Inviolata Itatiro na Anna Shanalingigwa.

Hata hivyo baada kupitiwa kwa kina rasimu katiba hiyo wameteuliwa wajumbe watatu kuingiza maboresho hayo na kuwapitisha tena wadau wao na maafisa Michezo walioelekezwa kabla ya kuipeleka kwa Msajili ili isajiliwe.

Aidha, Singo ameelekeza BMT kutangaza uchaguzi huo mapema wiki ijayo kwakuwa katiba ipo katika hatua za mwisho.

Maboresho ya rasimu ya katiba ya chama cha mchezo wa kuogelea nchini yamemuhusisha Mkurugenzi wa maendeleo ya Michezo Yusuph Singo, Kaimu Katibu Mkuu wa BMT na Msajili Ibrahim Mkwawa pamoja Katibu wa TSA Ramadhan Namkoveka na wajumbe wote wa kamati ya muda iliyoundwa kuandaa rasimu hiyo akiwemo, Mwenyekiti Alexander Mwaipai, Imani Ahmaya, Amina Mfaume,Inviolata Itatiro na Anna Shanalingigwa.

759 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/06/14/mkurugenzi-wa-maendeleo-ya-michezo-awataka-viongozi-wa-tsa-kutorudi-nyuma-wasimamie-maagizo-ya-waziri/">
RSS