DAR ES SALAAM MABINGWA COPA COCA COLA UMISSETA 2018.

Timu ya Mkoa wa Dar es salaam baada ya kukabidhiwa kombe la ubingwa la mashindano ya Copa Coca Cola UMISSETA 2018.
Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Mkoa wa Dar es salaam katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa kombe la ubingwa la mashindano ya Copa Coca Cola UMISSETA 2018.

Mashindano ya 39 Copa Coca Cola UMISSETA 2018, yamefikia tamati leo hii Juni 15, 2018 kwa timu ya mkoa wa Dar es Salaam kuibuka Bingwa wa jumla wa mashindano hayo kwa kujikusanyia jumla ya pointi 129.9 baada ya kutawala katika michezo mbalimbali kama vile riadha,mpira wa wavu,mpira wa miguu,mpira wa mikono,mpira wa pete na kuzipiku timu za mkoa wa Mwanza uliopata jumla ya pointi 118.8 na mkoa wa Tanga uliopata jumla ya pointi 92.7.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akikabidhi kombe la mshindi wa jumla wa mashindano ya UMISSETA 2018 timu ya mkoa wa Dar es Salaam (anayekabidhiwa kombe ni Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam Hamis Lisu)
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akikabidhi kombe la mshindi wa jumla wa mashindano ya UMISSETA 2018 timu ya mkoa wa Dar es Salaam (anayekabidhiwa kombe ni Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam Hamis Lisu)

Akizungumza wakati wa ufungaji wa mashindano hayo mkuu wa mkoa wa Mwanza Mheshimiwa John Mongela ameipongeza kampuni ya chapa ya Coca Cola kwa mchango wao mkubwa waliotoa kwa kushirikiana na serikali kufanikisha mashindano ya mwaka huu yaliyofanyika katika vituo vya shule ya sekondari Nsumba na chuo cha ualimu Butimba Jijini Mwanza.

“niwapongeze sana kampuni ya chapa ya Coca Cola kwa mchango wao mkubwa waliotoa kwa kushirikiana na serikali kufanikisha mashindano ya Mwaka huu,niwaombe msikate tamaa muendelee kudhamini mashindano haya ili vipaji Zaidi viendelee kuibuliwa”,Alisema Mh. Mongela.

IMG_3815Kwa upande wake mwakilishi wa kampuni ya Coca Cola Deus Kadico amesema wao kama Kampuni wataendelea kuunga mkono na kufadhili mashindano ya vijana kwa kuwa wanaamini, wanamichezo ni mabalozi wazuri wanaotangaza Taifa letu, vilevile wanao mtazamo wa kuibua na kukuza vipaji vya wanamichezo chipukizi nchini.

“mheshimiwa mgeni rasmi sisi kama kampuni tutaendelea kuunga mkono na kufadhili mashindano ya vijana kwa kuwa tunaamini wanamichezo ni mabalozi wazuri wanaotangaza Taifa letu, lakini pia tunao mtazamo wa kuibua na kukuza vipaji vya wanamichezo chipukizi nchini”, alisema Kadico.

258 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/06/15/dar-es-salaam-mabingwa-copa-coca-cola-umisseta-2018/">
RSS