HAKUNA BMT BILA VYAMA VYA MICHEZO

Kaimu Katibu mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Alex Nkenyenge amesema kuwa Baraza la Michezo la Taifa, lisingekuwepo bila ya vyama vya Michezo, hivyo Baraza litaonyesha ushirikiano kwa karibu ili kuhakikisha michezo inafanikiwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo miundombinu, vifaa na mafunzo endapo kama vyama vitatoa taarifa mapema kuhusu kile kinachoendelea kwenye chama husika.

Kaimu katibu mkuu wa BMT akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa maendeleo ya mchezo wa kriketi afrika pamoja na viongozi wa chama cha mchezo wa kriketi Tanzania.
Kaimu katibu mkuu wa BMT Alex Nkenyenge akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa maendeleo ya mchezo wa kriketi afrika pamoja na viongozi wa chama cha mchezo wa kriketi Tanzania.

Kaimu katibu mkuu ameyasema hayo tarehe 19 Juni, 2018, ofisini kwake alipotembelewa na kiongozi wa maendeleo ya mchezo wa kriketi kanda afrika Bi. Patricia Kambarami akiambatana na katibu wa fedha Kuben Rilvay pamoja na viongozi wa mchezo wa kriketi nchini Taher Kitisa (Mwenyekiti) na Zulfikar Rehemtulla (mtendaji mkuu).

“ninaamini kuwa Baraza bila vyama vya Michezo lisingekuwepo, hivyo basi vyama vya Michezo vinapaswa kulishirikisha baraza kile kinachoendelea katika chama husika ili kuhakikisha Michezo inafanikiwa katika Nyanja mbalimbali nchini ikiwemo miundombinu, vifaa na mafunzo”,alisema Nkenyenge.

IMG-20180620-WA0008Katika kikao hicho Bi. Patricia amesema wamekuja Tanzania kwa ajili ya kuongelea maendeleo ya mchezo wa kriketi na amekishukuru chama cha mchezo huo kwa kazi nzuri waliyoifanya kuhakikisha kuwa mchezo wa kriketi unafanya vizuri nchini.

“tumekuja Tanzania sio kwa ajili ya chama cha kriketi bali tumekuja kuongelea maendeleo ya mchezo wa kriketi, ila nikishukuru sana chama cha mchezo huu kwa kazi nzuri waliyoifanya kuhakikisha kuwa mchezo wa kriketi unafanya vizuri”, alisema Bi. Patricia.

432 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/06/19/hakuna-bmt-bila-vyama-vya-michezo/">
RSS