BMT LATHIBITISHA KUPOKEA KATIBA YA TSA

Baraza la Michezo la Taifa BMT kupitia katibu Mkuu Alex Nkenyenge, limethibitisha kupokea katiba ya chama cha mchezo wa kuogelea TSA, baada ya katiba hiyo kufanyiwa marekebisho kufuatia maelekezo ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Harrison G. Mwakyembe (Mb) aliyoyatoa tarehe 10 Juni, 2018 kwa viongozi wanaosimamia mchezo wa kuogelea nchini.

Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Alex Nkenyenge akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Uwanja wa Taifa,Tarehe 29 Juni 2018, kuhusu kupokelewa kwa katiba ya chama cha kuogelea Tanzania (TSA)
Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Alex Nkenyenge akizungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake Uwanja wa Taifa,Tarehe 29 Juni 2018, kuhusu kupokelewa kwa katiba ya chama cha kuogelea Tanzania (TSA)

Katibu Nkenyenge ameyathibisha hayo alipokuwa anazungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake tarehe 29 Juni 2018, ambapo amesema kuwa wakati wowote kuanzia Julai 2, 2018 Baraza linaweza kutangaza uchaguzi wa chama cha kuogelea ili kiweze kupata viongozi makini watakaoupeleka mchezo huo katika hatua nzuri ya maendeleo.

“kama ambavyo Mheshimiwa Waziri alivyotuagiza kusimamia chama cha kuogelea kuhakikisha kinapata katiba, tumefanya hivyo na chama hicho kupitia kamati ya muda wameweza kuwasilisha katiba tarehe 28 Juni 2018, na muda wowote kuanzia Julai 2, 2018 tutaweza kutangaza uchaguzi wa chama cha kuogelea ili chama kiweze kupata viongozi makini watakaoweza kuleta maendeleo mazuri katika mchezo wa kuogelea”,Alisema Nkenyenge.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt. Harrison G Mwakyembe (katikati) akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa pamoja 10 Juni, 2018, baina ya Serikali na viongozi wa zamani wa chama cha kuogelea nchini (TSA) kulia ni katibu Mkuu wa wizara, Susan Mlawi na Kushoto ni Kaimu katibu Mkuu wa BMT. Alex Nkenyenge.

Aidha katibu Nkenyenge amesema kwa kawaida katika chama cha kitaifa wanachama huwa ni vyama vya mkoa na kilichofanyika katika chama cha kuogelea kimetokana na wanachama wenyewe ambao wanakiu ya kuona mafanikio katika chama chao na mchezo wa kuogelea kwa ujumla.

“kwa kawaida katika chama cha kitaifa wanachana huwa ni vyama vya mkoa na kilichofanyika katika chama kimetokana na wanachama wenyewe ambao wanakiu ya kuona mafanikio katika mchezo wa kuogelea”,Alisema Nkenyenge.

55 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/06/29/bmt-lathibitisha-kupokea-katiba-ya-tsa/">
RSS