MWAKYEMBE: MICHUANO YA NDONDO KWA VIJANA INASAIDIA KUIBUA NA KUKUZA VIPAJI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mheshimiwa Harrison G Mwakyembe akikabidhi zawadi ya kombe kwa bingwa wa michuano ya kombe la Ndondo timu ya JK park baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya Bombom kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa uwanja wa JK park Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mheshimiwa Harrison G Mwakyembe akikabidhi zawadi ya kombe kwa bingwa wa michuano ya kombe la Ndondo timu ya JK park baada ya kufanikiwa kuifunga timu ya Bombom kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa uwanja wa JK park Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa dokta Harrison G. Mwakyembe,leo tarehe 1 Julai, 2018 amefunga mashindano ya kombe la Ndondo kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17, baada ya kushuhudia mtanange wa fainali kati ya timu ya JK park iliyokuwa inakipiga dhidi ya BomBom na JK kuchomoza na ushindi wa bao 1-0.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Harrison G Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Michezo, viongozi na wachezaji wa Timu ya BomBom Fc baada ya mechi ya kusaka mshindi wa tatu katika mashindano ya Ndondo Cup U17 2018 yaliyofanyika katika uwanja wa JK park Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Harrison G Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Michezo, viongozi na wachezaji wa Timu ya Kigamboni baada ya mechi ya kusaka mshindi wa tatu katika mashindano ya Ndondo Cup U17 2018 yaliyofanyika katika uwanja wa JK park Jijini Dar es salaam.

Akifunga mashindano hayo Dkt.Mwakyembe amesema, michezo kama ya Ndondo ni muhimu sana nchini kwani inasaidia kuibua vipaji vya wachezaji vipukizi, ambao ni hazina kubwa kwa Taifa kuwa na timu nzuri ya mpira wa miguu siku za usoni.

“nimeshuhudia mchezo mkali kweli, ambao unaonyesha jinsi gani timu zote mbili zimejipanga vizuri na wachezaji wanavipaji ambavyo vinaonekana, na kama nchi yetu katika kila mkoa ikiandaliwa michuano kama hii, nina uhakika kombe la dunia miaka ijayo tutashiriki”,alisema mh.Mwakyembe.

Aidha Dkt. Mwakyembe akusita kusisitiza suala la nidhamu kwa wachezaji, ambapo amesema kuwa nguzo kuu ya mafanikio kwa mchezaji wa mchezo wowote ule, ni nidhamu anapokuwa uwanjani na nje ya uwanja.

Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa, Alex Nkenyenge akikabidhi zawadi za mipira kwa timu shiriki za mashindano ya ndondo U17 2018.
Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa, Alex Nkenyenge akikabidhi zawadi za mipira kwa timu shiriki za mashindano ya ndondo U17 2018.

“niwaombe sana wachezaji bado mna safari ndefu katika mchezo huu wa mpira wa miguu, licha ya kuwa na vipaji vizuri, msipozingatia suala la nidhamu muwapo uwanjani na nje ya uwanja basi mtaharibikiwa na hamuwezi kufika mbali, hivyo basi mzingatie sana suala la nidhamu kwa ajili ya mafanikio zaidi”,alisisitiza Dkt.Mwakyembe.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), Wallace Karia amemuahidi Dkt. Mwakyembe kuwa watahakikisha mashindano ya kuibua vipaji vya vijana yanafanyika kila mwaka ili Taifa liweze kufikia malengo ya kuwa na wachezaji bora na wakulipwa ndani na nje ya nchi.

DSC_6706“nikuhakikishie Mheshimiwa Waziri tupo pamoja na wewe, na tutafanya kila kitu ambacho utatuagiza kufanya, tunakuahidi tutahakikisha mashindano kama haya yanafanyika kila mwaka ili Taifa liweze kufikia malengo ya kuwa na wachezaji bora na wakulipwa ndani na nje ya nchi”,Alisema Karia.

137 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/07/01/mwakyembe-michuano-ya-ndondo-kwa-vijana-inasaidia-kuibua-na-kukuza-vipaji/">
RSS