MWAKYEMBE: ROLL BALL SHIRIKIANENI NA VIONGOZI WA MAENDELEO YA MICHEZO KUUFIKISHA MCHEZO MBALI.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dokta Harrison G Mwakyembe ameuagiza uongozi wa chama cha mchezo wa Roll Ball kushirikiana kwa karibu na viongozi wa michezo nchini akiwemo Mkurugenzi wa maendeleo ya Michezo Yusuph Singo na kaimu katibu Mkuu wa BMT Alex Nkenyenge kuhakikisha kuwa mchezo huo unafanya vizuri katika Nyanja mbalimbali sanjari na kupata eneo la kuchezea mchezo huo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mheshimiwa Harrison G Mwakyembe  akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu katibu Mkuu wa BMT Alex Nkenyenge na viongozi wa chama cha mchezo wa Roll Ball, baada ya kikao maalum na viongozi wa chama kilichofanyika katika ukumbi wa uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Mheshimiwa Mwakyembe ameyasema hayo tarehe 2 Julai, 2018, katika kikao maalum na viongozi wa chama hicho pamoja na viongozi wa maendeleo ya michezo nchini, kilichofanyika katika ukumbi wa uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam, na kusema kuwa mchezo huo haupaswi kuchezwa na wanaume tu bali ata wanawake nao wahamasishwe ili kuweza kushiriki na kuuendeleza mchezo wa Roll ball.

“niwapongeze sana kwa jitihada nzuri mnazozifanya kama viongozi kuhakikisha mchezo huu unajulikana na kufika mbali, mmepiga hatua kubwa, lakini jaribuni kushirikiana na viongozi wa maendeleo ya michezo, mkurugenzi pamoja na Kaimu katibu wa BMT kuona ni jinsi gani wanawasaidia kupata sehemu ya kufanyia mazoezi,ila msikumbatie tu wanaume ata wanawake wapeni nafasi ya kuonyesha vipaji vyao katika mchezo huu”, alisema Dkt. Mwakyembe.

Mwenyekiti wa Chama cha mchezo wa Roll Ball Noeli Kiunsi akizungumzia nafasi adhimu waliyoipata kuonana na mheshimiwa waziri mwenye dhamana ya michezo, lengo kuu likiwa ni kuutambulisha mchezo wizarani ambao kwa sasa una miaka nane tangu uanzishwe licha ya kuwa na changamoto kama vile viwanja vya kuchezea pamoja na vifaa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha mchezo wa Roll Ball Noeli Kiunsi amesema amefurahishwa sana na nafasi adhimu waliyoipata kuonana na mheshimiwa waziri mwenye dhamana ya michezo, lengo kuu likiwa ni kuutambulisha mchezo wizarani ambao kwa sasa una miaka nane tangu uanzishwe licha ya kuwa na changamoto kama vile viwanja vya kuchezea pamoja na vifaa.

“tumefurahi sana kukutana na mheshimiwa waziri mwenye dhamana ya michezo ambaye ametuunganisha na mkurugenzi wa maendeleo ya Michezo ambaye atatupa muungozo wa kutumia viwanja vilivyopo ndani ya uwanja wa Taifa kuchezea mchezo wa Roll Ball,na nafikiri tutaanza hivi karibuni kwa ajili ya maandalizi hayo”, alisema Kiunsi.

126 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/07/02/mwakyembe-roll-ball-shirikianeni-na-viongozi-wa-maendeleo-ya-michezo-kuufikisha-mchezo-mbali/">
RSS