WAZIRI MWAKYEMBE AWATOA HOFU VIONGOZI WA TAVA WACHEZAJI WAO KUSAFIRI BILA KOCHA.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa nne kushoto akiwa kaitika picha ya pamoja na Viongozi wa mchezo wa Wavu Tanzania (TAVA) baada ya kikao nao Julai 2 mwaka huu, wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Michezo Yusuph Singo na wakwanza kulia ni Katibu Mkuu wa BMT Alex Nkenyenge.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa nne kushoto akiwa kaitika picha ya pamoja na Viongozi wa mchezo wa Wavu Tanzania (TAVA) baada ya kikao nao Julai 2 mwaka huu, wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Michezo Yusuph Singo na wakwanza kulia ni Katibu Mkuu wa BMT Alex Nkenyenge.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amewatoa hofu Viongozi wa chama cha mchezo wa Wavu nchini (TAVA) wachezaji wao kutosafiri bila kocha kwenda katika mashindano nchini Algeria yanayotarijiwa kuanza tarehe 19 hadi 25 mwezi Julai,2018 na kuwaahidi kufanya kila linanalowezekana ili vijana hao waweze kusafiri na kocha wao.

Mhe. Mwakyembe ameyasema hayo katika kikao na Viongozi wa mchezo huo kilichofanyika tarehe 2 Julai, 2018 katika Ofisi zake za Jijini Dar es salaam zilizopo uwanja wa Taifa, lengo la kikao hicho likiwa ni kusikiliza yale yanayoendelea katika chama hicho yakiwemo mafanikio na changamoto.

Timu ya wachezaji wawili wa kike wamelipiwa tiketi na kamati ya Olympiki Tanzania (TOC) wanatarajiwa kuondoka tarehe 16 mwezi huu kushiriki mashindano hayo, ambapo, viongozi wameeleza kuwa, timu ya wanaume na kocha hawatoweza kusafiri kutokana na kukosa pesa ya kuwasafirisha.

Mhe. Waziri amesema kuwa vijana hao hawawezi kusafiri bila mtu wa kuwasimamia na itaonekana kukosekana kwa umakini na kuwaahidi viongozi hao ataonge na viongozi wa TOC na atafanya kila namna kupata tiketi ya kocha na ikiwezekana na timu ya watoto wakiume iende .

“Wale ni watoto na kocha ni kama mlezi, tutaonekena hatuko makini, jamani lazima tujipange watoto waende na msindikizaji hata kama si kocha, lazima nihangaike,”alisema Mhe. Waziri.

Aidha, Dkt. Mwakyembe amesema katika kuifanya michezo ishirikishe watoto wote viongozi hao hawana budi kumsaidia kupiga kampeni kuhusu michezo mashuleni na kuyataka matawi ya mchezo huo kuleta taarifa ya shule ngapi hazitoi fursa kwa watoto kujiingiza katika michezo na kusema kuwa saikolojia ya makuzi ya mtoto hutokana na jinsi anavyoshiriki kucheza.

“Saikolojia ya makuzi ya mtoto hutokana na kucheza, tusaidiane pamoja kupiga kampeni kuhusu michezo mashuleni ili tuwe na viwango vya kimataifa,” alisisitiza.

Pia, Dkt. Mwakyembe katika suala la kiwanja ambalo viongozi hao wameeleza kukwama bandarini kwa takribani miaka mitatu kwa kukosa pesa ya kutolea kiasi cha milioni 18 hadi kufikia 53 amesema ataongea na kampuni iliyopisha kiwanja hicho, pamoja na kuwataka viongozi hao kuwasiliana na Vyombo vyenye dhamana ya michez mapema wanapoahidiwa kupata msaada wa vifaa vya mchezo ili hili lisijitokeze tena.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Alex Nkenyenge amewataka viongozi hao kuzingatia taratibu za uendeshaji wa chama kwa kuzingatia katiba na kuepuka kuifanya BMT kuwa mahakama.

Awali Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Yusuph Singo amewaeleza viongozi hao na wa vyama vingine kuwa serikali itatoa ushirikiano kwa viongozi wanaojituma kwa mambo mbalimbali ya kuendeleza chama.

Viongozi wa chama cha mchezo wa Wavu wakiongozwa na Mwenyekiti wao Meja Generali Mstaafu Peter Mlowezi katikati wakati wa kikao na Mhe. Mwakyembe.
Viongozi wa chama cha mchezo wa Wavu wakiongozwa na Mwenyekiti wao Meja Generali Mstaafu Peter Mlowezi katikati wakati wa kikao na Mhe. Mwakyembe.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa chama hicho, Meja Generali mstaafu Peter Mlowezi ameeleza kufurahisha na hatua za waziri katiak kikao hicho na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote ili kukijenga chama na mchezo.

 

 

78 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/07/02/waziri-mwakyembe-awatoa-hofu-viongozi-wa-tava-wachezaji-wao-kusafiri-bila-kocha/">
RSS