WAZIRI MWAKYEMBE: HATUJENGI TU KIWANJA LAKINI LAZIMA TUWE TUMEFIKIRIA NAMNA YA KUKITUNZA.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe amewaeleza Viongozi wa mchezo wa baseball nchini kufikiria namna ya kuutunza uwanja wa mchezo huo kabla ya kumalizika kujengwa ili kuepuka uharibifu wa mapema na kuufanya utumike kwa muda mrefu lakini pia kuepuka kuwakatisha tamaa wafadhili wa mradi huo.

Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo mheshimiwa Harrison G Mwakyembe akimshukuru Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida kuhusu mambo makubwa ambayo Serikali ya Japan imeshirikiana na Tanzania ukiwemo ujenzi wa uwanja bora wa mchezo wa BaseBall nchini uliopo katika shule ya sekondari Azania.
Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo mheshimiwa Harrison G Mwakyembe akimshukuru Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaharu Yoshida kuhusu mambo makubwa ambayo Serikali ya Japan imeshirikiana na Tanzania ukiwemo ujenzi wa uwanja bora wa mchezo wa BaseBall nchini uliopo katika shule ya sekondari Azania.

Hayo ameyasema tarehe 02 Julai, 2018 wakati alipotembelea uwanja wa mchezo huo uliopo katika shule ya Sekondari ya Azania, ambacho ni uwanja cha wazi uliotolewa na Manispaa ya Ilala unaojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan, ambapo, ziara aliyoifanya ilikuwa ni  kuona maendeleo ya ujenzi huo ulioanza Mei 3 na unatarajiwa kumalizika Agosti 15 mwaka huu.

“Hatujengi tu kiwanja lakini pia, lazima tuwe tunafikiria nanma ya kuutunza uwanja huo ili kuepuka uharibifu wa mapema, utumike kwa muda mrefu na tusiwakatishe tamaa wafadhili wetu,”alieleza Mhe. Mwakyembe.

Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo mheshimiwa Harrison G Mwakyembe akiangalia mchoro halisi wa uwanja wa BaseBall unaojengwa katika shule ya Sekondari ya Azania kwa ufadhili wa Serikali ya Japan.
Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo mheshimiwa Harrison G Mwakyembe akiangalia mchoro halisi wa uwanja wa BaseBall unaojengwa katika shule ya Sekondari ya Azania kwa ufadhili wa Serikali ya Japan.

Dkt. Mwakyembe alisema kuwa, Tanzania tunaupungufu mkubwa wa miundombinu ya michezo hivyo hatuna budi kuzitumia fursa zinazopatikana vizuri na kuishukuru Serikali ya Japan ambayo imekuwa ikishirikiana na nchi yetu katika mambo mengi ambapo sasa wameingia kwenye michezo kwa udhamini wa mashindano kama riadha ya wasichana na vilevile kuanza kwa ujenzi wa kiwanja cha mchezo baseball ambao ni mpya Tanzania lakini umesambaa Mikoa mingi kwa msaada wa wataalam kutoka Japan.

Lakini pia, amewapongeza Viongozi wa mchezo huo kwa ushirikiano walionao na wafanyabiashara wa nchi hiyo wakiwemo Konoike na wengine ambao wamekuwa na mchango mkubwa kwa nchi yetu.

Kaimu Katibu Mkuu wa BMT Alex Nkenyenge akitoa maelekezo kwa mwenyekiti wa chama cha mchezo huo Dokta Ahmed Makata.
Kaimu Katibu Mkuu wa BMT Alex Nkenyenge akitoa maelekezo kwa mwenyekiti wa chama cha mchezo huo Dokta Ahmed Makata.

Katika hatua nyingine Mhe. Mwakyembe amechukukizwa na mwingiliano uliopo baina ya eneo la shule na wananchi waliojenga pembezoni waopita humo na kupelekea ukuta kuvunjwa, hali itakayopelekea uwanja na vifaa vya mchezo huo kutokuwa salama, na kumtaka Mkuu wa shule ya Sekondari Azania Erasto Gwimile kumwandikia maelezo kuhusu hilo ili ashauriane na Mawaziri husika na Mkuu wa Mkoa kuona namna sahihi ya usalama wa eneo hilo.

Aidha, katika suala hilo alieleza kuwa, lazima ukuta ujengwe na hata kama pesa haitapatikana yuko tayari kupitisha harambe ili ukuta ujengwe na kuwataka wanaofanya shughuli zao eneo hilo kuondoke haraka sana ambako amemtaka mwalimu Mkuu wa shule hiyo kuwaandikia watu hao barua ya kuwataka kuondoka mahali hapo ili kuilinda shule na miundombinu hiyo ya mchezo wa baseball.

baseball 1“Mimi nitakuja hapa na Mkuu wa Mkoa na Viongozi wote, haya mambo tunayalea, hawa jamaa lazima waondoke na haya magari kama hawayahitaji tutakarabati yakawa ya shule, turudishie ukuta wetu Mogadishu watajua pakwenda, hakuna uungwana, Serikali haina uungwana unaovunja sheria lazima waondoke”alisisitiza Dkt. Mwakyembe.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Kisutu na Mjumbe wa chama cha mchezo wa baseball Kheri Kessy alisema kuwa anamwomba Waziri afanyie kazi ombi la Mkuu wa shule kujengewa uzio kwani si wakazi wa Mogadishu tu waopita hapo kwani wapo wengine wanapita kwa kupitisha vitu vya kihalifu kwa maana wakiingia eneo la shule wanaonekana wako salama lakini wakitoka wanaendelea na uovu wao.

Awali msimamizi wa ujenzi wa uwanja huo kutoka Manispaa ya Ilala Bi. Leila Omary alieleza kwa kina maendeleo ya ujenzi huo na kusema kuwa pamajo na changamoto ya mvua iliyojitokeza na kusababisha shughuli zingine kutoendelea lakini kutokana na ushirikiano uliopo kati ya Manispaa, Chama cha Baseball na Serikali ya Japan amemuhakikishia Waziri kazi hiyo itakamilika kwa wakati.

135 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by EmailO
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/07/02/waziri-mwakyembe-hatujengi-tu-kiwanja-lakini-lazima-tuwe-tumefikiria-namna-ya-kukitunza/">
RSS