WAZIRI MWENYE DHAMANA YA MICHEZO AVITAKA VYAMA VYA MICHEZO KUFIKISHIA TAKWIMU ILI AJIVUNIE KWA MAKUBWA WANAYOFANYA.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amevitaka Vyama vya Mchezo kufikisha takwimu za mambo mengi mazuri wanayofanya pamoja na  wachezaji mbalimbali wanaofanya vyema katika mashindano  ya kitaifa na kimataifa, taarifa ambazo angezitumia kujivunia katika hotuba zake tofauti ikiwemo wakati wa bunge.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akitoa maelekezo kwa chama cha mchezo wa mashua juu ya uandishi wa mipango ya chama.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akitoa maelekezo kwa chama cha mchezo wa mashua juu ya uandishi wa mipango ya chama.

Rai hiyo ameitoa wakati wa kikao chake na Viongozi wa chama cha mchezo wa Mashua (TSAA) ikiwa ni ratiba yake aliyojiwekea kuhakikisha mwaka unapoisha anakutana na vyama vyote vya michezo ili kujifunza na kuelewa mambo tofauti yanayoendelea katika michezo yakiwemo mafanikio na  changamoto mbalimbali zinazokabili maendeleo ya michezo nchini ili kuzitafutia ufumbuzi, kikao kilichofanyika katika moja ya kumbi za uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Lakini pia Dkt. Mwakyembe amewataka Viongozi hao  kuwasilisha kwa Serikali mipango ya chama ya muda mfupi na mrefu ili ufuatiliaji wa mipango hiyo uwe kwa urahisi kwa wahusika,

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo watatu kushoto katika picha ya pamoja na Viongozi wa mchezo wa mashua baada ya kumaliza kikao nao jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo (watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa mchezo wa mashua baada ya kumaliza kikao nao jijini Dar es salaam kulia ni Mkurugenzi wa Michezo Yusuph Singo na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa BMT  Alex Nkenyenge.

“Hebu jitahidini kuwa mnawasilisha takwimu za mambo mengi mazuri mnayofanya pamoja za wachezaji mbalimbali wanaofanya vyema katika mashindano ya kitaifa na kimataifa ambapo, nitajivunia katika hotuba zangu tofauti ikiwemo bungeni, lakini wasilisheni pia mipango yenu ya muda mfupi na mrefu ili tuweze kufanya ufuatiliaji na watendaji wangu,”alieleza Waziri Mwakyembe.

Dkt. Mwakyembe alisema hayo baada kupewa taarifa za vijana wa kitanzania wanamashua wanaotarajia kuiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia na Afrika, akiwemo   Mstr. Saidi Halfan Mkomba moja kati ya vijana wawili wa Afrika watakaoiwakilisha katika mashindano yatakayofanyika Julai 9 hadi 21 Mjini Texas nchini Marekani. Vilevile  katika mashindano ya Afrika (IODA) nchini Maputo – Mozambique Tanzania itawakilishwa na Janeth P. Nassari, Khultum H. Kassinge, Peter C. Msotwa, Abdallah A. Amanzi na William M. Leah katika mashindano yanayotarajiwa kufanyika tarehe 13 hadi 23 mwezi Septemba.

Kaimu Katibu mkuu BMT Alex Nkenyenge akitoa maelekezo namna kuandika andiko lililiojitosheleza kuhusu miundombinu ya mchezo huo.
Kaimu Katibu mkuu BMT Alex Nkenyenge akitoa maelekezo namna kuandika andiko lililiojitosheleza kuhusu miundombinu ya mchezo huo.

Aliendelea kuwa suala na miundombinu ya mchezo huo ambayo imependekezwa kujengwa eneo la Msasani atakutana Waziri wa maliasili, ardhi, Mifugo na Uvuvi, Tamisemi ambapo atatakiwa Mkuu wa Mkoa, na Ofisi ya Rais Mazingira, ambapo Mhe. Mwakyembe amesema wakikaa kwa pamoja hilo linafanikiwa.

Hata hivyo Viongozi hao wameelekezwa kuandaa andiko linalojitosheleza ili kufanyikisha hilo na kuliwasilisha mapema Baraza la Michezo la Taifa na kwa Mkurugenzi.

Kwa upande wake Mwenyekiti  wa (TSAA) amemshukuru Waziri Mwakyembe kwa hatua aliyofikia na kumhakikishia Waziri kuiwasilisha taarifa hiyo mapema.

Kikao cha Dkt. Mwakyembe kilimhusisha Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Yusuph Singo, Kaimu Katibu Mkuu wa BMT Alex Nkenyenge pamoja na Viongozi wa chama cha Mashua akiwemo Mwenyekiti Philimon Nassari na Wajumbe ni Mwambao Helef, Joyce Charles na Halife Mpondi.

 

 

 

 

736 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/07/03/waziri-mwenye-dhamana-ya-michezo-avitaka-vyama-vya-michezo-kufikishia-takwimu-ili-ajivunie-kwa-makubwa-wanayofanya/">
RSS