DKT. MWAKYEMBE AFURAHISHWA NA RASIMU YA KATIBA YA NGUMI ZA KULIPWA KUZINGATIA AFYA NA MASLAHI YA WACHEZAJI.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Yusuph Singo (kushoto) na Kaimu Katibu Mkuu wa BMT wakimsikiliza Katibu wa Kamati ya muda wa ngumi za kulipwa wakati akiwasilisha rasimu ya katiba Julai 6, 2018 ukumbi wa habari Maelezo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa, na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Yusuph Singo (kushoto) na Kaimu Katibu Mkuu wa BMT Alex Nkenyenge kulia wakimsikiliza Katibu wa Kamati ya muda wa ngumi za kulipwa Yahya Poli hayupo kwenye pichawakati akiwasilisha rasimu ya katiba Julai 6, 2018 ukumbi wa habari Maelezo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameeleza kufurahishwa na rasimu ya Katiba ya ngumi za kulipwa kuzingatia afya za wachezaji pamoja na maslahi yao na kusema kuwa itakapopitishwa na kusajiliwa itawatia moyo vijana wengi sana kujiunga na mchezo huo, vilevile itaipa nguvu Serikali kusimamia mchezo wa ngumi za kulipwa nchini. Rasimu iliyoandaliwa na kamati ya muda aliyoiunda mwanzoni mwa mwaka huu kusimamia mchezo huo kwa kushirikiana na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) huku wakiandaa rasimu hiyo.

Dkt. Mwakyembe ameeleza hayo, tarehe 16 Julai, 2018 wakati alipofanya kikao na kamati hiyo kwa muda wa zaidi ya saa tano kwa kupitia rasimu ya katiba ya ngumi hizo hatua kwa hatua ili baadaye ipelekwe kwa wadau wake na hatimaye kusajiliwa na kuwa rasmi kutumika katika mchezo huo nchini. Kikao kilichokaliwa ukumbi wa Habari Maelezo uliopo katika jengo lenye kumbi za kimataifa la Julius Nyerere lililopo jijini  Dar es salaam.

“Nimefurahi sana, nimeona hii rasimu ya katiba imetambua umuhimu wa afya za wachezaji wa mchezo huu, siyo afya tu bali hata maslahi yao yamezingatiwa vizuri sana, mimi najua hii katiba ikishapitishwa itawatia moya vijana wengi sana kuingia katika mchezo huu, vilevile inatupa nguvu sana sisi upande wa Serikali kuongeza nguvu zaidi katika kusimamia ngumi za kulipwa nchini,”alisema Waziri Mwakyembe.

Aliendelea kuwa, Tanzania sasa umezaliwa mchezo wa ngumi za kulipwa baada ya kukaa  na kuipitia rasimu hiyo yenye kurasa 19 kipengele kwa kipengele na kuona imesheheni mambo mengi muhimu yatakayowasaidia wachezaji wa ngumi hizo na Serikali  katika kuusimamia mchezo huo.

Aidha, Mhe. Waziri ameeleza kuwa, itaposajiliwa katiba ya ngumi hizo na kuchaguliwa uongozi mpya, viongozi hao lazima washirikiana na wale wa ngumi za ridhaa kwani bila kufanya hivyo itaendelea kuwepo vurugu katika ngumi nchini na kueleza kuwa, Serikali haitakubali suala hilo kuwepo tena kwani mchezaji hawezi kufika ngumi za kulipwa bila kuanzia kwenye ngumi za ridhaa.

“Bila ushirikiano wa ngumi za kulipwa na ngumi za ridhaa tutaendelea na vurugu ambazo hatuwezi kukubali, haiwezekani mtu anatokea na kuanza na ngumi za kulipwa, ngumi hizi ni hatua ya juu lazima uwe umefanya kazi ngazi ya chini ambayo ni ngumi za ridhaa na umetambulika na kuna vigezo umefikia, hii haiwezekani,”alisema Mhe. Mwakyembe.

Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa Waziri wakati wa kupitia rasimu ya katiba ya ngumi za kulipwa wa kwanza kushoto ni Katibu wa Kamati Yahya Poli wakimsikiza Wazir Mwakyembe hayupo pichana akitoa maelekezo kuhusu rasimu hiyo.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa Waziri wakati wa kupitia rasimu ya katiba ya ngumi za kulipwa wa kwanza kushoto ni Katibu wa Kamati Yahya Poli wakimsikiza Waziri Mwakyembe hayupo pichani akitoa maelekezo kuhusu rasimu hiyo.

Hata hivyo, Mhe. Mwakyembe ameipongeza sana kamati kwa kazi kubwa waliyoifanya isiyo na malipo kwani hata wakilipwa haitalingana na kazi kubwa waliyoifanya na kuwataka Wajumbe wa Kamati hiyo  kuingiza marekebisho machache aliyoelekeza na kuandaa mkutano wake na wadau wa ngumi hizo mwishoni mwa mwezi huu ili kuwapitisha na hatimaye kusajiliwa na kuelekea katika uchaguzi mkuu wa chombo hicho nchini.

Kwa upande wake Katibu wa Kamati hiyo na mtaalamu wa sheria Yahya Poli amemuahidi Mheshimiwa waziri kuyafanyia kazi maboresho machache aliyowaelekeza na kuitisha mkutano wa wadau katika kipindi alichoagiza kufanyika kwa mkutano huo.

 

733 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/07/06/dkt-mwakyembe-afurahishwa-na-rasimu-ya-katiba-kuzingatia-afya-na-maslahi-ya-wachezaji/">
RSS