UCHAGUZI WA TGU KUFANYIKA 18 AGOSTI, 2018.

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limetangaza uchaguzi wa chama cha mchezo wa Gofu (TGU) unaotarajiwa kufanyika Tarehe 18 Agosti, 2018 katika klabu ya Gymkhana mkoani Morogoro.

Afisa Habari wa Baraza la Michezo la Taifa Bi Najaha Bakari akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu Uchaguzi wa chama cha mchezo wa Gofu (TGU).
Afisa Habari wa Baraza la Michezo la Taifa Bi Najaha Bakari akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu Uchaguzi wa chama cha mchezo wa Gofu (TGU).

Akitangaza uchaguzi huo mbele ya waandishi wa habari leo hii 26 Julai, 2018, katika moja ya kumbi za uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam, Afisa Habari wa BMT Najaha Bakari amesema fomu zitaanza kutolewa bure katika ofisi za Baraza zilizopo uwanja wa Taifa, na pia kupatikana katika tovuti ya Baraza ambayo ni www.nationalsportscouncil.go.tz, kuanzia tarehe 26 hadi 16 Agosti, mwaka 2018.

Aidha Afisa Najaha amesema usaili utafanyika tarehe 17 Agosti, 2018 siku moja kabla ya uchaguzi, halafu tarehe 18 Agosti utaanza kufanyika mkutano mkuu, kisha uchaguzi wenyewe.

Nafasi zinazogombewa ni;

  1. Rais (President)
  2. Makamu wa Rais (Vice President)
  3. Katibu wa Heshima (Hon. Secretary)
  4. Mweka Hazina (Hon. Treasurer)
  5. Katibu Mshindani (Competition Secretary)
  6. Handicap Secretary

Kwa upande wa sifa za wagombea ambao watajitokeza kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo, Afisa Najaha amesema kiongozi lazima awe na sifa zifuatazo:

  1. Awe ni Raia wa Tanzania
  2. Awe na uzoefu wa uongozi pamoja na taaluma za uongozi wa Michezo.
  3. Awe na ujuzi wa mchezo wa Mpira wa Magongo.
  4. Awe hajatenda kosa lolote la Jinai.

Aidha afisa Najaha ametoa wito wito kwa wadau wote wenye sifa na wenye nia njema ya kuendeleza mchezo wa Gofu nchini kujitokeza kwa wingi kuchukuwa fomu, ili waweze kupatikana viongozi bora.

 

100 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/07/26/uchaguzi-wa-tgu-kufanyika-18-agosti-2018/">
RSS