NKENYENGE: ONGEZENI JUHUDI KUUPANUA MCHEZO WA MBIO ZA MAGARI MIKOANI ILI KUWEZA KUPATA VIPAJI ZAIDI.

Kaimu katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Alex Nkenyenge amekitaka chama cha mchezo wa mbio za magari nchini, kuangalia fursa na uewezekano wa kuendeleza mchezo huo hasa kwa vijana wadogo katika ngazi za shule za msingi na sekondari sanjari na kuongeza juhudi za kuupanua mchezo katika mikoa mingine ya Tanzania ili kuweza kupata vipaji zaidi.

Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Alex Nkenyenge (mwenye shati la kitenge) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama cha mchezo wa mbio za magari pamoja na washiriki wa mafunzo ya usalama barabarani kutoka katika mikoa mbalimbali Tanzania.
Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Alex Nkenyenge (mwenye shati la kitenge) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama cha mchezo wa mbio za magari Tanzania na Afrika Kusini sanjari na washiriki wa mafunzo ya usalama barabarani kutoka katika mikoa mbalimbali Tanzania.

Katibu Nkenyenge ameyasema hayo tarehe 28 Julai, 2018, alipokuwa anafunga kozi ya mafunzo ya usalama kwa waendesha magari ya mashindano,ufungaji uliofanyika katika moja ya kumbi za Gymkhana jijini Dar es salaam, ambapo amesema ni hatua kubwa kwa chama kuweza kuendesha mafunzo hayo kwani usalama ni kitu cha kwanza unapoendesha chombo cha moto barabarani.

“ni hatua kubwa kwa chama cha mchezo wa mbio za magari ambao usalama ni kitu cha kwanza, kwa hiyo wamefanya vyema kuendesha kozi ya usalama kwa waendesha magari pamoja na viongozi wa vilabu mbalimbali ambao wametoka katika mikoa ya Tanga,Iringa, Morogoro, Arusha, Dar es salaam na Mwanza,” Alisema Nkenyenge.

Kaimu Katibu Mkuu wa BMT Alex Nkenyenge akimkabidhi Bi. Hidaya Kamanga hati ya ushiriki wa mafunzo ya usalama barabarani kwa waendesha magari yaliyoandaliwa na chama cha mchezo wa mbio za magari nchini (AAT)
Kaimu Katibu Mkuu wa BMT Alex Nkenyenge akimkabidhi Bi. Hidaya Kamanga hati ya ushiriki wa mafunzo ya usalama barabarani kwa waendesha magari yaliyoandaliwa na chama cha mchezo wa mbio za magari nchini (AAT)

Aidha katibu Nkenyenge amewataka viongozi waliopata mafunzo hayo, kuitumia vyema fursa hiyo kuweza kuwafundisha wengine, kwani si wote waliopata nafasi ya kuweza kuhudhuria mafunzo hayo yaliyotolewa na wataalam kutoka chama cha mchezo wa mbio za magari duniani ambao kwa tawi la barani afrika wametokea nchini afrika kusini.

“nyinyi viongozi ambao mmepata mafunzo haya, basi ni vyema mkaitumia fursa hiyo kuwafundisha wengine ambao hawakuweza kufika hapa katika mafunzo haya muhimu yaliyotolewa na wataalam hawa kutoka chama cha mchezo wa mbio za magari duniani ambao kwa tawi la barani afrika wametokea nchini afrika kusini,” Alisema Nkenyenge.

Kaimu Katibu Mkuu wa BMT Alex Nkenyenge akimkabidhi Mosi Makau hati ya ushiriki wa mafunzo ya usalama barabarani kwa waendesha magari yaliyoandaliwa na chama cha mchezo wa mbio za magari nchini (AAT)
Kaimu Katibu Mkuu wa BMT Alex Nkenyenge akimkabidhi Mosi Makau hati ya ushiriki wa mafunzo ya usalama barabarani kwa waendesha magari yaliyoandaliwa na chama cha mchezo wa mbio za magari nchini (AAT)

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa (AAT) Yusuf A. Ghor amesema wameamua kuendesha mafunzo hayo ili kuweza kuwapa waendesha magari na viongozi mbalimbali elimu ya mipango ya usalama barabarani hususani usalama kwa watembea kwa miguu, viongozi wa mbio pamoja na madaktari wa huduma ya kwanza katika mashindano.

“tumeamua kuendesha mafunzo haya ili kuweza kuwapa waendesha magari na viongozi mbalimbali elimu muhimu ya mipango ya usalama barabarani, hususani usalama kwa watembea kwa miguu, viongozi wa mbio pamoja na madaktari wa huduma ya kwanza katika mashindano,”alisema Gor.

46 total views, 3 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by EmailO
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/07/28/nkenyenge-ongezeni-juhudi-kuupanua-mchezo-wa-mbio-za-magari-mikoani-ili-kuweza-kupata-vipaji-zaidi/">
RSS