SHIRIKIANENI KWA UKARIBU NA TFF KUYATANGAZA MASHINDANO YA AFCON U17, 2019

Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Susan Mlawi, amevitaka vyombo vya Habari nchini kushirikiana kwa ukaribu na shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kuyatangaza na kuwaelewesha wananchi juu ya mashindano ya AFCON U17 ambayo Tanzania itakuwa mwenyeji mwaka 2019.

Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Susan Mlawi akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari za Michezo kuhusu kuyatangaza mashindano ya AFCON U17 2019 ambayo Tanzania ndio mwenyeji, anayefuata Pembeni Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya maendeleo ya Michezo Yusuf Singo na Katibu wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF)  Wilfred Kidau.
Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Susan Mlawi akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari za Michezo kuhusu kuyatangaza mashindano ya AFCON U17 2019 ambayo Tanzania ndio mwenyeji, anayefuata Pembeni Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya maendeleo ya Michezo Yusuf Singo na Katibu wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) Wilfred Kidau.

Katibu Mlawi ameyasema hayo tarehe 6 Agosti, 2018 katika kikao chake na wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari, kilichofanyika katika moja ya kumbi za uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam, ambapo Bi. Mlawi amesema kuyatangaza mashindano hayo kutasaidia kuleta hamasa kubwa kwa mashabiki na wadau wa michezo nchini kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia timu ya Taifa ili iweze kufanya vizuri.

“Ndugu wahariri wa vyombo vya Habari za michezo nchini niwaombe mshirikiane kwa ukaribu na TFF kuyatangaza na kuwaelewesha wananchi juu ya mashindano ya AFCON U17 ambayo sisi ndio waandaaji mwakani, kwani kwa kuyatangaza kutasaidia kuleta hamasa kubwa kwa mashabiki na wadau wa michezo nchini kujitokeza kwa wingi uwanjai kuishangilia timu ya Taifa ili iweze kufanya vizuri”,alisema Bi. Susan.

FB_IMG_1474866862644Aidha Bi. Susan amesema mashindano ya AFCON U17 ni mashindano makubwa na ya kihistoria kwa nchi ya Tanzania ambayo yataleta sifa kubwa kwa Taifa kujitangaza kimataifa, hivyo serikali kwa kushirikiana na TFF watahakikisha kuwa maandalizi yanafanyika vizuri ili mashindano yaweze kufana na timu yetu ya vijana kuweza kufanya vizuri.

“haya ni mashindano makubwa na ya kihistoria kwa nchi yetu ambayo yatatupa sifa kubwa na kujitangaza kimataifa, hivyo kwa kuona umuhimu wa mashindano haya, serikali kwa kushirikiana na TFF tutahakikisha kuwa maandalizi yanafanyika vizuri kwani tulikwisha thibitisha uwepo wake”, alisema Bi. Susan.

“katika kuhakikisha maandalizi yanafanyika vizuri, waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, aliteua kamati yenye wajumbe 25 anayoiongoza yeye mwenyewe, kamati hii inaendelea na vikao vya maandalizi kwa kupanga mipango mbalimbali ili michezo iendeshwe kwa ufanisi, kama nchi mwenyeji ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa wageni wanaingia nchini salama, michezo inachezwa salama na wanaondoka kurejea makwao salama”,alisema Bi. Susan.

 

96 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/08/06/shirikianeni-kwa-ukaribu-na-tff-kuyatangaza-mashindano-ya-afcon-u17-2019/">
RSS