TIMU NNE (4) KUIWAKILISHA TANZANIA MASHINDANO YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Idara ya maendeleo ya michezo kwa kushirikiana na Baraza la Michezo la Taifa, limeteua timu nne (4) zitakazosafiri kwenda kushiriki katika mashindano ya Jumuiya ya Afrika mashariki yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi tarehe 16 hadi 30, Agosti 2018, katika jiji la Bunjumbura nchini Burundi.

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Yusuf Singo akizungumza na viongozi wa timu zilizoteuliwa kwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yatakayofanyika jijini Bunjumbura nchini Burundi, pembeni ni Kaimu katibu mkuu wa BMT Alex Nkenyenge akisikiliza alichokuwa anakizungumza mkurugenzi.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Yusuf Singo akizungumza na viongozi wa timu zilizoteuliwa kwenda kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yatakayofanyika jijini Bunjumbura nchini Burundi, pembeni ni Kaimu katibu mkuu wa BMT Alex Nkenyenge akisikiliza alichokuwa anakizungumza mkurugenzi.

Akizungumza katika kikao na viongozi wa timu hizo kilichofanyika tarehe 10 Agosti, 2018 katika moja ya kumbi za uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Yusuf Singo amesema wameteua timu ya Mpira wa Miguu wanawake (wachezaji 20 na viongozi 5), Netiboli (wachezaji 12 na viongozi 2), Riadha (wachezaji 8 na viongozi 2) na Karate (wachezaji 4 na kiongozi 1) kulingana na ufinyu wa Bajeti uliopo, hivyo anaamini timu hizo zilizochaguliwa ni timu zenye upinzani na zinaenda Burundi kushindana na sio kushiriki.

“Tumeteua timu ya mpira wa Miguu wanawake yenye wachezaji 20 na viongozi 5, Timu ya Netiboli wachezaji 12 na viongozi 2, Riadha wachezaji 8 na viongozi 2 na Karate wachezaji 4 na kiongozi 1, tungependa tupeleke timu nyingi zaidi lakini kulingana na ufinyu wa bajeti hatutaweza, hivyo tunaamini kuwa timu tulizozichagua zinaupinzani mkubwa na zinaenda huko kushindana na sio kushiriki”, alisema Singo.

Baadhi ya viongozi wa vyama wakisikiliza kwa makini alichokuwa anazungumza Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Yusuf Singo kuhusu safari ya kwenda Burundi kwenye mashindano.
Baadhi ya viongozi wa vyama wakisikiliza kwa makini alichokuwa anazungumza Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Yusuf Singo kuhusu safari ya kwenda Burundi kwenye mashindano.

Aidha mkurugenzi Singo amesema endapo kama mambo yatakwenda kama yalivyopangwa timu hiyo ya watu 60 itaondoka nchini kuelekea nchini Burundi tarehe 14 Agosti, 2018, ambapo msafara huo utaondoka kwa usafiri wa Barabarani licha ya uchovu watakaokuwa nao wachezaji lakini bado kuna uwezekano mkubwa wa timu hizo kufanya vizuri.

Kwa upande wake mmoja wa viongozi wa timu ya karate nchini Wilson Ringo amepongeza juhudi zinazoonyeshwa na wizara kupitia Idara ya Maendeleo ya Michezo pamoja na BMT kuelekea katika mashindano hayo ya jumuiya ya Afrika Mashariki sanjari na kutoa ushauri kwa serikali kuhusu suala la waamuzi watakaokuwa wanachezesha mashindano hayo.

“Niipongeze sana wizara kwa juhudi inazoonyesha kuelekea katika mashindano haya ya jumuiya ya Afrika Mashariki, lakini pia niiombe serikali kuangalia suala la waamuzi kama inawezekana twende na waamuzi wetu hili kuwe na uiano mzuri wa waamuzi na kuepusha upendeleo”, alisema Ringo.

9 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/08/10/timu-nne-4-kuiwakilisha-tanzania-mashindano-ya-jumuiya-ya-afrika-mashariki/">
RSS