NKENYENGE: MAMBO YOTE NA MAFANIKIO YANAYOONEKANA YANAANZA NA MAMA.

Wanawake washiriki wa mafunzo ya uongozi yaliyofanyika Agosti, 21 kwa uratibu wa BMT na TPC katika ukumbi wa uwanja wa Uhuru jijin Dar es salaam.
Wanawake washiriki wa mafunzo ya uongozi yaliyofanyika Agosti, 21 kwa uratibu wa BMT na TPC katika ukumbi wa uwanja wa Uhuru jijin Dar es salaam.

Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Alex Nkenyenge ameeleza kuwa, mambo yote na mafanikio yanayoonekana yanaanza na mama kwa namna moja au nyingine kwani mama ni mlezi wa familia na ndiyo kila kitu.

Hayo ameyaeleza tarehe 21 Agosti, 2018 wakati alipokuwa akifunga mafunzo na kugawa vyeti kwa wanawake wahitimu wa mafunzo ya uongozi wa michezo, mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

“Mambo yote na Mafanikio yanayoonekana lazima yametokana na mwanamke kwa namna moja au nyingine,mama ndiyo mlezi wa familia na mama ndiyo kila kitu,”alieleza Nkenyenge.

Hata hivyo amewataka wahitimu hao ambao wengi wao ni watu wenye ulemavu kuwapa moyo na kuwashauri wanawake wenye watoto wenye ulemavu kuwapa nafasi watoto wao kushiriki katika michezo, lakini pia kuwapa moyo wanawake wengine wenye ulemavu wa wasiokuwa na ulemavu kushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi kwa kuamini kuwa mwanamke ndio kila kitu.

IMG_8108Kaimu Katibu Mkuu wa BMT akimkabidhi cheti Sikujua Mbwembwe moja ya wahitimu wa mafunzo ya uongozi wa michezo kwa wanawake yaliyofanyika Agosti 21, 2018 kwa uratibu wa BMT kwa ushirikiano na Kamati ya wachezaji wenye ulemavu nchini (TPC) jijini Dar es salaam.

Aidha, Nkenyenge ameeleza kufurahisha na mafunzo hayo kuja kwa wakati muafaka ambapo wanawake wameanza kupata ujuzi na maarifa yanayoendana na uongozi na kusema kuwa haiwezekani kwa namna yoyote mtu akachaguliwa kuwa kiongozi bila kuonekana anafanya kitu na kusema kuwa lazima atoke aonekane anafanya kitu ndiyo achaguliwe.

“Haiwezekani kwa namna yoyote ukachaguliwa bila kuonekana unafanya kitu, kwahiyo lazima utoke uonekane unafanya kitu ndiyo uchaguliwe,”alisema.

Lakini pia amewataka wahitimu hao na hasa wenye ulemavu kutokata tamaa kwa kukaa kulia na kuwaeleza kwamba haitawasaidia ambapo aliwaasa kwa kuwaasa kuwa ulemavu siyo sababu ya kutofanya kazi nyingine na machozi hayatabadili hali. vilevile amewata kuwahamasisha wenzao wenye ulemavu kujihusisha na michezo pamoja na uongozi, lakini pia kuutumia ujuzi waliopata katika sehemu wanazotoka kwa faida ya jamii.

“Tusikate tamaa na ulemavu wa viungo siyo sababu ya kutofanya, wala kukaa na kulia hakutabadili hali,suala la msingi tuwape moyo wenzetu  na tuutumie ujuzi na maarifa uliyopata yasibaki yako peke yako iwe faida kwa jamii, kwani maarifa ni Zaidi ya uwezo,”alisisitiza Nkenyenge.

Kwa upande wake mhitimu na Mwl. wa shule ya watu wenye ulemavu jeshi la uokovu Juliana alieleza kuwa mafunzo aliyopata yamemsaidia sana na kuahidi kusema kuwa hatabaki kuwa mwalimu pekee bali ifikapo mwaka wa uchaguzi kwa TPC 2018 lazima afanye maamuzi ya kugombea.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu wa Kamati ya Paralimpiki Tanzania (TPC) Tuma Dandi alieleza kuwa, pamoja na uwepo wa changamoto ya vifaa na pesa ya kutoa mafunzo katika Mikoa yote, TPC itajitahidi kufanya kila linalowezekana kupanua mafunzo hayo kwa wanawake wengi Zaidi nchini.

Mkufunzi wa mafunzo ya uongozi ya wanawake kwa watu wenye ulemavu kutoka BMT Neema Msita akitoa mafunzo kwa wanawake washiriki wa mafunzo hayo Agosti 21 jijini Dar es salaam.
Mkufunzi wa mafunzo ya uongozi ya wanawake kwa watu wenye ulemavu kutoka BMT Neema Msita akitoa mafunzo kwa wanawake washiriki wa mafunzo hayo Agosti 21 jijini Dar es salaam.

 

 

 

89 total views, 3 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/08/21/nkenyenge-mambo-yote-na-mafanikio-yanayoonekana-yanaanza-na-mama/">
RSS