NKENYENGE AWATAKA WACHEZAJI WA GOFU KUIWAKILISHA VYEMA NCHI KWA USHINDANI NA SIYO KUSHIRIKI

gofu 1Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Alex Nkenyenge akikabidhi bendera kwa Mwenyekiti wa TLGU Sophia Viggo ili kuelekea nchini Ghana katika mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kuanza tarehe 29 mwezi huu hadi tarehe 4 Septemba, 2018.

Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Alex Nkenyenge amewataka wachezaji wa chama cha mchezo wa gofu ya wanawake kuiwakilisha vyema nchi kwa kushindana na siyo kwenda kushiriki katika mashindano hayo na kuleta kikombe au midali, mashindano  yanayotarajiwa kufanyika nchini Accra Ghana  kuanzia tarehe  29 Agosti hadi tarehe 4 Septemba yatakayohusisha nchi 26 za Afrika.

Haya ameyasema tarehe 26 Agosti, 2018 wakati wa kuikabidhi bendera timu hiyo ya gofu ya wanawake inayoshiriki katika mshindano hayo nchini Ghana ikiwa na wachezaji watatu na kiongozi mmoja wanaosafiri jumatatu tarehe 27 saa kumi alfajiri, tukio lililofanyika katika ukumbi wa uwanja wa uhuru jijimi Dar es salaam.

“Kaiwakilisheni vyema nchi yetu kwa kwenda kushindana na siyo kushiriki, mkashindane na inawezekana kabisa kuleta kikombe kwani nina uhakika timu inayoenda ni timu ya uhakika iliyochujwa na tuna mabingwa wengi ambao wangeweza kuwakilisha lakini kwakuwa bajeti haikutosha hawa wachache tunaamini wataibeba bendera ya Taifa  na kuipeperusha vyema,”alisema Nkenyenge.

Aidha, Nkenyenge amewashukuru wale wote waliofanikisha safari ya timu hiyo na kusema kuwa ni zaidi ya zawadi kwa wachezaji na watanzania lakini pia ni wajibu wa watanzania wote kuweza kusaidiana ili tuweze kusonga mbele zaidi kimaendeleo. Lakini pia amewatakia kwa niaba ya BMT na Serikali kwa ujumla amewatakia safari, wawe na afya njema pamoja na kufanya kile ambacho watanzania wamewatuma.

“Mnakwenda kuna watu zaidi ya milioni hamsini na tano ambao mmewabeba migongini mwenu, usijiangalie kama mchezaji binafsi lakini jiangalie kama nchi,” alisema.

Naye Mwenyekiti wa chama cha gofu cha wanawake Tanzania (TLGU) Sophia Viggo amesema kuwa watanzania wasiwe na hofu wachezaji wake wamepata muda wa kujiandaa vizuri hivyo watarejea na medali.

Kwa upande wake nahodha wa timu hiyo, Madina Iddy amewaomba watanzania waendelee kuwaombea pamoja kuwatoa hofu kwa kuahidi kufanya vizuri kwani wamejiandaa vizuri na kusema kuwa nchi wanazoenda kushindano nazo wanazimudu zote ingawa mshindani wawo mkubwa ni Afrika ya kusini lakini wamejipanga kutoa.

Wachezaji wanaoiwalisha nchi katika mashindano hayo ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika nchini Acra Ghana kuanzia tarehe 29 mwezi huu hadi tarehe 4 Septemba, 2018 ni Hawa Wanyeche, Angel Eaton,na Madina Iddy wakiambatana na kiongozi ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha gofu cha wanawake nchini (TLGU) Sophia Viggo.

 

 

 

 

 

 

62 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/08/26/nkenyenge-awataka-wachezaji-wa-gofu-kuiwakilisha-vyema-nchi-kwa-ushindani-na-siyo-kushiriki/">
RSS