MAENDELEO YA MCHEZO HUU YAMEKWAMISHWA NA UROHO NA UBINAFSI WA BAADHI YA WADAU WA NGUMI ZA KULIPWA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison G. Mwakyembe amewaeleza wadau wa ngumi za kulipwa kuwa maendeleo ya mchezo huo yamekwamishwa na uroho na ubinafsi wa baadhi ya wadau wa mchezo huo wasiopenda maendeleo ya wengine.

IMG_8676

Hayo ameyasema leo tarehe 27 Agosti, 2018 katika mkutano na wadau wa ngumi za kulipwa nchini wakiwemo mabondia, wakuzaji, mawakala na kamati aliyoiunda mwanzoni mwa mwaka huu kuandaa rasimu ya katiba itakayoweza kukidhi matakwa ya wadau wa ngumi hizo ili kuijadili kwa pamoja na kuipitisha rasimu hiyo kabla ya kusajiliwa na kuanza kutumika rasmi, mkutano ulifanyika katika ukumbi wa uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam.

“Maendeleo ya mchezo huu yamekwamishwa kwa muda mrefu na  ubinafsi na uroho wa baadhi ya watu wa ngumi za kulipwa, hilo lazima niliseme wazi, wizi wizi tu nimeliona hilo ndugu zangu,”alieleza kwa masikitiko na kuongeza kuwa:

IMG_8690

“Tumeshafika mahali kwa ajili ya uroho tu kuifanya nchi yetu ni ngazi ya kupandishia hadhi mabondia wa nchi za nje bila mabondia wetu kujiandaa, haiwezekani lazima vijana wetu wajiandae kimazoezi na kisaikolojia, hii ni nchi ya neema mungu ametupa kipaji,”alisema

“Pesa ambayo wanalipwa vijana wangu ni ndogo sana, tumefanya utafiti sitaki hata kusema hapa ni aibu pesa ndogo sana, pambano la dola kadhaa kijana analipwa dola mia tano na ubabaishaji mwingi kuwa unajua ningekulipa dola elfu moja lakini nakulipia chakula cha kwenye ndege, unatumia choo mule vitu ambavyo havina gharama, tiketi nimekulipia mwenyewe wakati wanaoandaa pambano hilo wameshalipa, haya mambo yanawafanya vijana wetu wawe maskini haiwezekani lazima mabadiliko yafanyike,”

IMG_8612

Aliendelea kuwa, hiki ni kipindi cha mabadiliko lazima mabadiliko yafanyike na mwakani lazima kutakuwa na mabadiliko makubwa katika mchezo wa ngumi za kulipwa nchini, ambapo alieleza kuwa mungu ametoa kipaji cha mchezo huo nchini lazima kitumike.

Aidha Dkt. Mwakyembe amesisitiza kuwa mabadiliko yatakayofanyika katika mchezo wa ngumi za kulipwa ni lazima mabondia walipwe haki yao kulingana na kile wanachostahili, ili wasizidi kuitangaza nchi kimataifa huku wakiendelea kuwa maskini.

IMG_8599

Mheshimiwa Waziri alisema kuwa ngumi ni kati ya michezo michache Tanzania ambayo tumeonyesha kipaji cha hali ya juu ndani na nje ya nchi kwa kuwa na mabondia wazuri sana, lakini maisha yao bado hafifu kwa sababu ya uonevu uliokuwa ukifanywa huko nyuma, tumekuwa na mabondia wazuri kama vile Rashid matumla, Hassan matumla, Francis Cheka, Kalama nyilawila na wengine wengi, lakini ukiangalia maisha yao hivi sasa bado hawajafikia kiwango cha juu kwa sababu ya uonevu sasa lazima tubadilike.

8 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/08/27/maendeleo-ya-mchezo-huu-yamekwamishwa-na-uroho-na-ubinafsi-wa-baadhi-ya-wadau-wa-ngumi-za-kulipwa/">
RSS