UCHAGUZI WA CHABATA KUFANYIKA OCTOBA JIJINI DODOMA

Waendesha baiskeli wakiwa katika moja ya mashindano ya mchezo huo nchini.
             Waendesha baiskeli wakiwa katika moja ya mashindano ya mchezo huo nchini.

Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha mchezo wa baiskeli Tanzania (CHABATA) unatarajiwa kufanyika Octoba 06 Jijini Dodoma chini ya uratibu na usimamizi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).

Fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa chama hicho zinapatikana katika Ofisi za Baraza zilizopo uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na katika tovuti ya BMT ambayo ni www.nationalsportscouncil.go.tz na zinaanza kutolewa kuanzia leo tarehe 30 Agosti, na mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu hizo ni tarehe 01 Octoba, 2018.

Aidha, usaili wa wagombea wa nafasi mbalimbali za uchaguzi huo utafanyika tarehe 05 Octoba kuanzia saa 3:00 asubuhi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo siku inayofuata huko Dodoma, ambapo, mahali wagombea na wapiga kura watafahamishwa kabla ya kufika tarehe hizo.

Nafasi zinazogombewa ni nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu, ada ya fomu kwa nafasi hizi ni sh. 50,000. Nafasi nyingine ni za wajumbe sita (6) wakuchaguliwa huku wakitakiwa kulipia ada ya fomu sh.30,000.

Hatahivyo kulingana na katiba ya chama cha mchezo huo mgombe anatakiwa kuwa awe na elimu ya kidato cha nne au zaidi, taaluma na uzoefu wa uongozi katika mchezo wa baiskeli, raia wa Tanzania na awe hajawahi kuhusika katika kosa lolote la jinai au kufungwa jela kwa kipindi kisichopungua miezi sita

BMT inatoa wito kwa wenye nia ya dhati ya maendeleo ya mchezo huo, wana vigezo vyote vya kuwa kiongozi waone umuhimu wa kuchukua fomu na kugombea nafasi stahiki ili kuendeleza chama na mchezo wa baiskeli nchini.

Fomu zinatakiwa kulipiwa akaunti ya Baraza kwa jina la “National Sports Council Ac. No. 20401100013” na kuwasilishwa risiti iliyolipiwa Benki pamoja fomu zilizojazwa kwa umakini.

 

 

 

 

 

 

89 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/08/30/uchaguzi-wa-chabata-kufanyika-octoba-jijini-dodoma/">
RSS