AKHWARI AWASHAURI WATANZANIA KUTOKATA TAMAA

Nguli wa Riadha aliyelitangaza Taifa kimataifa kupitia mchezo wa Riadha miaka ya sitini (60) Mzee John Stephen Akhwari amewashauri watanzania kupitia sekta zote kutokata tamaa na kusema kuwa kujituma na kuonesha uzalendo kuna faida yake.

Mzee John Stephen Akhwari akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu katibu Mkuu wa BMT Makoye Alex Nkenyenge (aliyevaa tai nyekundu) ofisini kwa Katibu BMT.
Mzee John Stephen Akhwari akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu katibu Mkuu wa BMT Makoye Alex Nkenyenge (aliyevaa tai nyekundu) ofisini kwa Katibu BMT.

Hayo ameyasema leo 6 Septemba, 2018 alipotembelea Ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na kukutana na Kaimu Katibu Mkuu pamoja na wafanyakazi wa BMT huku akiwaeleza mengi yanayomfanya atambulike kimataifa, baada ya baadhi ya nchi kuutumia usemi wake aliousema katika michezo ya olimpiki iliyofanyika nchini Mexico alipoumia na kuambiwa apande gari lakini alikataa na kuendelea na mbio hizo kwa kusema “nchi yangu haikunituma kuanza mbio hizo bali na kuzimaliza pia”

“kila mtu katika kila unachofanya hutakiwi kukata tamaa kwani huenda kuna faida ndani yake na uzalendo ni kitu cha muhimu ndiyo maana nilipoumia katika michezo ya Olimpiki iliyofanyika mwaka 1968 nchini Mexico waliniambia nipande gari nisiendelee na mbio hizo, lakini niliwaambia “nchi yangu haikunituma kuanza mbio bali na kuzimaliza pia”, alisema Mzee Akhwari.

IMG_8982Vilevile, Mzee Akhwari katika mazungumzo yake na Kaimu Katibu Mkuu wa BMT Makoye Alex Nkenyenge alishauri jamii kuwa na kawaida ya kuweka kumbukumbu na matukio muhimu huku akiishauri Serikali kuweka kumbukumbu za wafanyakazi wake wanaofanya vizuri siyo viongozi wakuu pekee, lakini pia kuweka kumbukumbu za wanamichezo wanalitangaza taifa kimataifa kupitia michezo mbalimbali. Alisema hayo akirejea yanayofanya na baadhi ya nchi kumuenzi yeye baada ya kuwa zinatumia kauli yake hiyo katika sehemu tofauti ikiwemo wakati wa kufundisha michezo na hata sehemu za ibada huku akisisitiza watu kutokata tamaa.

Aliongeza kuwa, mwishoni mwa mwezi Agosti kutokana na nchi ya Mexico kuweka kumbukumbu zake za miaka 50 baada ya Olimpiki iliyofanyika mwaka 1968 wakati alipotoa kauli hiyo, wakiazimisha miaka 50  tangu kufanyika kwa michezo hiyo walimwalika kuhudhuria sherehe hizo.

IMG_9184Awali Nkenyenge alimweleza Mzee Akhwari kufurahishwa na ujio wake nguli huyo wa riadha katika Ofisi za baraza na kusema kuwa katika kile kinachofanyika kwa ajili yake kinaweza kuwekwa vizuri zaidi kwakuwa kama kuna taarifa zimekosekana ataziweka yeye vizuri. Lakini pia alimweleza kuwa kitabu cha historia yake alichoahidiwa kipo kwenye hatua nzuri na kitakapokamilika watanzania watamfahamu zaidi kwa kupata kumbumbuku zake katika andiko hilo.

IMG_8965 (2)John Stephen Akhwari ni mzaliwa wa Wilaya ya Mbulu sehemu ambayo hali yake ya hewa ni nzuri kwa michezo na hasa kwa kuandaa wanariadha na wengi waliofanya vizuri kitaifa na kimataifa wanatoka ukanda huo, lakini pia,  mwanariadha huyo sifa yake ya kutokata tamaa imemfanya atambulike kimataifa.

6 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/09/06/akhwari-awashauri-watanzania-kutokata-tamaa/">
RSS