NKENYENGE AWATAKA WATANZANIA KUTUMIA FURSA KUELEKEA AFCON U17 2019

Kaimu katibu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Makoye Alex Nkenyenge amewataka watanzania kutumia fursa iliopo nchini kuelekea katika michuano ya kombe la mataifa Barani Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka kumi na saba (Afcon U17) 2019 itakayofanyika katika uwanja wa Taifa na Azam Complex Jijini Dar es Salaam.

Kaimu katibu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Makoye Alex Nkenyenge akiwataka watanzania kutumia fursa iliopo nchini kuelekea katika michuano ya kombe la mataifa Barani Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka kumi na saba (Afcon U17) 2019
Kaimu katibu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Makoye Alex Nkenyenge akiwataka watanzania kutumia fursa iliopo nchini kuelekea katika michuano ya kombe la mataifa Barani Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka kumi na saba (Afcon U17) 2019

Nkenyenge ameyasema hayo tarehe 17 Septemba, 2018 alipokuwa anazungumza na vyombo vya Habari ofisini kwake uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo amesema michuano ya Afcon U17 2019 ni fursa kwa watanzania kiuchumi na kijamii, hivyo ni wakati sahihi sasa kwa mtanzania mmoja mmoja katika kila nafasi yake kuitumia fursa hii kutangaza bidhaa na huduma walizonazo ili kujinufaisha na kulitangaza Taifa kimataifa.

“Michuano ya Afcon U17 ni fursa kwa watanzania kiuchumi na kijamii, hivyo ni wakati sahihi kwa mtanzania mmoja mmoja katika kila nafasi yake kuitumia fursa hii kutangaza bidhaa za huduma walizonazo ili kujinufaisha na kulitangaza Taifa kimataifa,”alisema Nkenyenge.

Akifafanua kuhusu suala la matumizi ya mara kwa mara ya uwanja wa Taifa kuelekea michuano ya Afcon U17 2019, Nkenyenge amesema Serikali ya awamu ya Tano imetenga fedha kufanya matengenezo ya viwanja vitakavyotumika lakini pia kupitia matumizi ya uwanja wa Taifa yanafanya wataalam kufahamu changamoto zilizopo na kuzifanyia marekebisho kwa uimara zaidi kuelekea katika michezo hiyo.

“ndugu waandishi, Serikali yetu ya awamu ya tano ipo makini sana na imetenga fedha kwa ajili ya kufanya matengenezo na wataalam wapo wanaendelea na matengenezo ya viwanja vitakavyotumika baada ya kugundua changamoto zilizopo vinapotumika,”alisema Nkenyenge.

Katika hatua nyingine Kaimu Katibu wa BMT alipoulizwa kuhusu uchaguzi wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), amesema taratibu za katiba ya BFT zipo katika hatua za mwisho ofisi ya Msajili, zitakapokamilika itasajiliwa na uchaguzi utatangazwa ili kuweza kupata viongozi halali watakaoongoza shirikisho hilo.

 

592 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by EmailO
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/09/17/nkenyenge-awataka-watanzania-kutumia-fursa-kuelekea-afcon-u17-2019/">
RSS