UCHAGUZI WA SHIRIKISHO LA MIELEKA KUFANYIKA 27 OKTOBA, 2018.

Baraza la Michezo la Taifa (BMT), limetangaza uchaguzi wa viongozi wa Shirikisho la Mieleka ya Ridhaa Tanzania (TAWF) unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Oktoba, 2018 katika ukumbi wa msasani bichi klabu, jijini Dar es Salaam.

Afisa Habari wa BMT Frank Mgunga akitangaza uchaguzi wa viongozi wa Shirikisho la Mieleka ya Ridhaa Tanzania (TAWF) unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Oktoba, 2018 katika ukumbi wa msasani bichi klabu, jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari wa BMT Frank Mgunga akitangaza uchaguzi wa viongozi wa Shirikisho la Mieleka ya Ridhaa Tanzania (TAWF) unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Oktoba, 2018 katika ukumbi wa Msasani bichi klabu, jijini Dar es Salaam.

Akitangaza uchaguzi huo Afisa Habari wa BMT Frank Mgunga amesema fomu zitaanza kutolewa katika ofisi za Baraza na pia kupatikana katika tovuti ambayo ni www.nationalsportscouncil.go.tz kuanzia tarehe 17 Septemba, 2018 ambapo mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni tarehe 19 Oktoba, 2018.

Aidha usaili, utafanyika tarehe 26 Oktoba kuanzia saa 3:00 asubuhi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo siku inayofuata na mahali mtafahamishwa kabla ya kufika tarehe hizo.

Kwa upande wa nafasi zinazogombewa Mgunga amesema nafasi hizo ni pamoja na Rais, Makamu Rais ambapo katika nafasi hizi mbili ada yake ya kuchukua fomu ni sh. 50,000, huku nafasi nyingine kama vile Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mhasibu Mkuu, Afisa Habari na wajumbe watatu(3) wa kuchaguliwa ada ya fomu ni sh. 30,000, ambapo fomu zilipiwe katika akaunti ya Baraza kwa jina la National Sports Council Ac. No. 20401100013 na kuwasilisha BMT fomu zilizojazwa kwa usahihi.

Katika hatua nyingine Mgunga amesema wagombea wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi huo wa TAWF wanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:

  1. Awe mwanachama wa Shirikisho la Mieleka Nchini (TAWF)
  2. Awe na umri wa kuanzia miaka 25 na kuendelea.
  3. Asiwe amewahi kupatikana na kosa la jinai.
  4. Kwa nafasi ya Rais, Makamu wa Rais, Katibu Mkuu na Msaidizi, awe na elimu ya kidato cha nne na kuendelea pamoja na uwezo wa kuandika na kusoma kingereza na kiwasahili kwa ufasaha.
  5. Awe na akili timamu.
  6. Mhasibu Mkuu na Msaidizi awe na cheti cha uhasibu, Stashahada au zaidi ya hapo.
  7. Sifa za wajumbe wa kamati mbalimbali wawe na uzoefu wa mchezo wa mieleka, wanaojua sheria za mchezo wa mieleka au wawe wameshawahi kuwa viongozi katika ngazi ya vilabu, wilaya, mkoa na Taifa.
  8. Asiwe amewahi kucheza, kuongoza au kushiriki kwa namna yoyote ile mieleka ya kulipwa.

BMT limetoa wito kwa wenye nia ya dhati ya kuendeleza mchezo wa mieleka, kujitokeza kuchukua fomu na kugombea nafasi stahiki ili kuendeleza Shirikisho pamoja na kuiletea sifa nchi.

 

242 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/09/17/uchaguzi-wa-shirikisho-la-mieleka-kufanyika-27-oktoba-2018/">
RSS