UFAFANUZI WA KAMATI YA KUSIMAMIA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI KUHUSU BONDIA HASSAN MWAKINYO

Kamati ya kusimamia ngumi za kulipwa nchini, imetoa ufanunuzi kuhusu suala la bondia Hassan Mwakinyo ambaye majuma mawili yaliyopita alilipa sifa kubwa Taifa baada ya kumtwanga bondia Sam Eggington kwa TKO raundi ya pili katika pambano la raundi 10 lisilo la ubingwa lililofanyika tarehe 8 Septemba, 2018 huko Birmingham, Uingereza.

Katibu wa kamati ya ngumi za kulipwa Yahya Poli akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu suala la Bondia Hassan Mwakinyo kusafiri nje ya nchi bila kibali ambapo amesema si kweli kwamba Bondia Mwakinyo alisafiri kwenda nchini Uingereza bila kibali kama alivyodai katika vyombo vya Habari
Katibu wa kamati ya ngumi za kulipwa Yahya Poli akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu suala la Bondia Hassan Mwakinyo kusafiri nje ya nchi bila kibali ambapo amesema si kweli kwamba Bondia Mwakinyo alisafiri kwenda nchini Uingereza bila kibali kama alivyodai katika vyombo vya Habari.

Akizungumza na waandishi wa Habari tarehe 17 Septemba, 2018, Katibu wa kamati ya ngumi za kulipwa Yahya Poli amesema si kweli kwamba Bondia Mwakinyo alisafiri kwenda nchini Uingereza bila kibali kama alivyodai katika vyombo vya Habari, wakala aliyekwenda na Mwakinyo aliwasilisha maombi yake ya safari hiyo ndani ya siku saba (7) kabla ya safari ambapo kamati iliyajadili na kupitia kumbukumbu mbalimbali za Mwakinyo pamoja na mpinzani wake na kuridhia kumwombea kibali ili aweze kusafiri kwa ajili ya pambano hilo.

Katibu wa kamati ya kusimamia Ngumi za kulipwa Tanzania, Yahya Poli akionyesha barua ya kuomba kibali na Kibali chenyewe cha Bondia Hassani Mwakinyo kilichotolewa na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ili bondia huyo aelekee nchini Uingereza kwa ajili ya pambano la ngumi dhidi ya bondia Sam Eggington.

“maombi ya kibali toka katika kamati kwenda BMT yaliwasilishwa tarehe 3 Septemba,2018 kwa maombi ya dharura na tarehe 5 Septemba, 2018 kibali kilitolewa na nakala yake kutumiwa wakala aliyewasilisha maombi hayo ndugu Rashid Nassor ambaye ndiye aliyesafiri naye siku hiyo, ikumbukwe kwamba kwa mujibu wa kanuni za BMT, maombi ya vibali vya kusafiri nje ya nchi kwa shughuli za kimichezo yanapaswa kuwasilishwa siku 14 kabla ya safari, napenda kusisitiza kwamba, Hassan Mwakinyo alipata kibali kama nilivyoelekeza na nichukue fursa hii kumwomba radhi Katibu wa BMT pamoja na watendaji wote kwa kadhia waliyoipata”,alisema Poli.

Boxing - Arena BirminghamAidha Poli amesisitiza kuwa suala la viza kwa mchezaji ni jukumu la promota na wakala/ bondia mwenyewe na pesa hiyo huwa inarudishwa na promota wanapofika huko kwenye pambano, hivyo kamati inasikitika kwa changamoto aliyoipitia kupata viza lakini inaamini kuwa wamerudishiwa na labda wakala aliyekwenda naye ndugu Rashid Nassor atalitolea ufafanuzi suala hilo atakaporudi.

“napenda ifahamike kwamba, suala la visa ni jukumu la promota na wakala/ bondia mwenyewe na pesa hiyo kuwa inarudishwa na promota wanapofika huko kwenye pambano, hivyo tunasikitika kwa changamoto hiyo aliyoipata kupata visa lakini tunaamini kuwa wamerudishiwa na labda wakala aliyekwenda naye ndugu Rashid Nassor anaweza kulitolea ufafanuzi zaidi”, alisema Poli.

 

307 total views, 2 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by EmailO
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/09/17/ufafanuzi-wa-kamati-ya-kusimamia-ngumi-za-kulipwa-nchini-kuhusu-bondia-hassan-mwakinyo/">
RSS