JUKUMU LA BMT NI KUSIMAMIA NA KUSAIDIA VYAMA KUTEKELEZA MAKUJUMU YAO.

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kupitia Afisa Michezo Neema Msitha akimwakilisha Katibu Mtendaji wa BMT Makoye Alex Nkenyenge, amesema jukumu la BMT ni kusimamia na kusaidia vyama kutekeleza majukumu yao, hivyo vyama inabidi kufanya shughuli zao kwa kuzingatia sheria ya Baraza pamoja na katiba zao.

Afisa Michezo wa BMT Neema Msitha akizungumza na vyombo vya habari kuhusu jukumu la BMT ambalo ni kusimamia na kusaidia vyama kutekeleza majukumu yao, hivyo vyama inabidi kufanya shughuli zao kwa kuzingatia sheria ya Baraza pamoja na katiba za vyama vyao.

Neema ameyasema hayo tarehe 22 Septemba, 2018 alipohudhuria katika mashindano ya wazi ya kuogelea Tanzania, yaliyofanyika katika shule ya kimataifa ya Tanganyika upanga jijini Dar es Salaam, ambapo amesema suala la kuendeleza michezo ni jukumu la vyama, hivyo ni vyema kujipanga kuwa na mipango endelevu inayoonekana ili kuweza kushawishi Umma kuwekeza katika michezo nchini.

IMG_0360“jukumu la BMT ni kusimamia na kusaidia vyama kutekeleza majukumu yao, hivyo vyama inabidi kufanya shughuli zao kwa kuzingatia sheria ya Baraza pamoja na katiba za vyama vyao na suala la kuendeleza michezo ni jukumu la vyama, hivyo ni vyema vyama kujipanga kuwa na mipango endelevu inayoonekana ili kuweza kushawishi Umma kuwekeza katika michezo nchini”,alisema Neema.

Aidha Neema ametoa wito kwa vyama vya michezo nchini kuendesha mashindano ya kitaifa kwa ajili ya kuendeleza vipaji vilivyoibuliwa kutoka katika vilabu na mikoa mbalimbali nchini.

IMG_0623Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la kuogelea Tanzania (TSA) Imani Alimanya amesema ni muda mfupi sana tangu uongozi huo uingie madarakani, lakini wamejitahidi kuandaa mashindano hayo ambayo wanaamini kuwa ndio chakula kikubwa kwa muogeleaji kujipima na kuongeza bidii zaidi ili kuweza kufanya vizuri kitaifa na kimataifa.

Rais wa Shirikisho la kuogelea Tanzania (TSA) Imani Alimanya akizungumza na waandishi wa Habari na kusema kuwa ni muda mfupi sana tangu uongozi huo uingie madarakani, lakini wamejitahidi kuandaa mashindano hayo ambayo wanaamini kuwa ndio chakula kikubwa kwa muogeleaji kujipima na kuongeza bidii zaidi ili kuweza kufanya vizuri kitaifa na kimataifa.

“ukiangalia mpaka sasa ni muda mfupi sana tangu tuingie madarakani, lakini tumejitahidi kuandaa mashindano haya ambayo tunaamini kuwa ndio chakula kikubwa kwa muogeleaji kujipima na kuongeza bidii zaidi ili wachezaji wetu waweze kufanya vizuri kitaifa na kimataifa”,alisema Alimanya.

IMG_0391Ata hivyo Alimanyama amesema hatua inayofuata kwa sasa wanajiandaa na mashindano ya Cana Zone III yanayotarajiwa kufanyika mwezi Novemba, 2018 nchini Sudan.

1,894 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by EmailO
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/09/22/jukumu-la-bmt-ni-kusimamia-na-kusaidia-vyama-kutekeleza-makujumu-yao/">
RSS