BMT LAIPONGEZA TOC KWA JITIHADA ZA KUSHIRIKI MICHEZO YOTE INAYOANDALIWA NA IOC

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kupitia Afisa Michezo Benson Chacha, limeipongeza Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kwa jitihada ilizozionyesha kushiriki katika michezo yote inayoandaliwa na Kamati ya Olimpiki Kimataifa (IOC).

Afisa Michezo wa BMT, Benson Chacha, akizungumza na vyombo vya Habari kuipongeza Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kwa jitihada ilizozionyesha kushiriki katika michezo yote inayoandaliwa na Kamati ya Olimpiki Kimataifa (IOC).
Afisa Michezo wa BMT, Benson Chacha, akizungumza na vyombo vya Habari kuipongeza Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kwa jitihada ilizozionyesha kushiriki katika michezo yote inayoandaliwa na Kamati ya Olimpiki Kimataifa (IOC).

Chacha ameyasema hayo katika kikao na waandishi wa Habari kilichofanyika tarehe 28 Septemba, 2018, wakati wa kuiaga Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka kumi na nane (U18) inayoondoka tarehe 3 Oktoba,2018, kwenda kushiriki katika mashindano ya Olimpiki 2018, kwa vijana chini ya umri wa miaka kumi na nane (U18) nchini Argentina.

“Niipongeze sana TOC kwa kufanya jitihada kuhakikisha inashiriki katika michezo yote inayoandaliwa na kamati ya olimpiki kimataifa (IOC), huu ni mfano wa kuigwa kwa vyama vingine vya michezo nchini kuhakikisha vinaandaa mashindano mbalimbali ya ndani na kujitahidi kushiriki katika michezo ambayo inaandaliwa na mashirikisho ya kimataifa”,alisema Chacha.

IMG_0977

Aidha Chacha amewapongeza wanamichezo ambao wamefuzu kwenda kushiriki katika mashindano hayo ya Olimpiki kwa Vijana, kwani katika michezo arobaini na nane (48) nchini ni michezo miwili tu (Riadha na Kuogelea) ambayo wachezaji wetu wameonekana wana sifa kushiriki katika mashindano hayo.

Kwa upande wake katibu wa TOC, Filbert Bayi amesema michezo hiyo ya vijana ilianza kwa mara ya kwanza mjini Singapore 2010, na Tanzania iliweza kushiriki tangu mchezo wa kwanza ikiwa na wachezaji wanne (4) wa Timu za kuogelea pamoja na Riadha kwa sababu ndio michezo pekee ambayo imekuwa ikishiriki mara kwa mara katika mashindano ya dunia.

Katibu wa TOC, Filbert Bayi akizungumza na vyombo vya Habari kuelezea michezo ya vijana Olimpiki iliyoanza kwa mara ya kwanza mjini Singapore 2010, na Tanzania iliweza kushiriki tangu mchezo wa kwanza ikiwa na wachezaji wanne (4) wa Timu za kuogelea pamoja na Riadha
Katibu wa TOC, Filbert Bayi akizungumza na vyombo vya Habari kuelezea michezo ya vijana Olimpiki, iliyoanza kwa mara ya kwanza mjini Singapore 2010, na Tanzania iliweza kushiriki tangu mchezo wa kwanza ikiwa na wachezaji wanne (4) wa Timu za kuogelea pamoja na Riadha.

“michezo hii ya vijana ilianza kwa mara ya kwanza mjini Singapore 2010, na nchi yetu iliweza kushiriki tangu mchezo wa kwanza ikiwa na wachezaji wanne (4) wa timu za kuogelea na riadha kwa sababu ndio michezo pekee ambayo imekuwa ikishiriki mara kwa mara katika mashindano ya dunia”,alisema Bayi.

Nae Rais wa TOC, Gulam Rashid akikabidhi bendera ya Taifa kwa wachezaji wanaokwenda kushiriki katika mashindano ya Olimpiki kwa vijana chini ya umri wa miaka kumi na nane (U18), amewataka viongozi na wachezaji kuhakikisha kwamba wanafikia viwango vya kushindana katika mashindano ya kimataifa na kuipeperusha vyema bendera ya Taifa katika michezo mbalimbali duniani.

 

516 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/09/28/bmt-laipongeza-toc-kwa-jitihada-za-kushiriki-michezo-yote-inayoandaliwa-na-ioc/">
RSS