DKT. MWAKYEMBE: BMT WAITENI TASWA NA WAWAKILISHI WA WAANDISHI PITIENI KATIBA IFANYIWE MABORESHO KABLA YA KUELEKEA KATIKA UCHAGUZI

 

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiwaeleza jambo Waandishi wa habari za Michezo (hawapo pichani) wakati wa kikao nao leo tarehe 02 Octoba, 2018 alipowaita kuongea nao, tukio lililofanyika katika moja ya kumbi za uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiwaeleza jambo Waandishi wa habari za Michezo (hawapo pichani) wakati wa kikao nao leo tarehe 02 Octoba, 2018 alipowaita kuongea nao, kushoto ni Mkurugenzi wa Michezo Yusuph Singo na kulia ni Afisa habari TFF Cliphody Ndimbo, tukio lililofanyika katika moja ya kumbi za uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka watendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuwaita Viongozi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) pamoja na wawikilishi wa Waandishi wa habari za michezo ambao siyo wanachama wa TASWA ili kupitia  kwa pamoja Katiba ya chama hicho na kuifanyia maboresho yanayoendana na wakati, lakini pia kuwaita wadau wote kuipitia na kusajiliwe kabla ya kuelekea katika uchaguzi wa chama hicho.

Rai hiyo ameitoa leo Octoba 2, 2018 wakati wa kikao chake na Waandishi wa habari za michezo alichokiitisha baada ya kupokea barua na simu nyingi kufuatia changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo na kudai kutopata msaada kwa Chama kinachowasimamia.

“BTM waiteni TASWA na wawakilishi wa waandishi wa habari za michezo ambao siyo wanachama muipitie katiba kwa makini iendane na wakati na kuiwasilisha kwa wadau wote,  isajiliwe kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi,”alisema Waziri Mwakyembe.

Waziri baada kuwasikiliza wengi wa Waandishi hao wakiwa na nia kuunda chombo kingine aliwashauri kuwa, kuundwa kwa chombo kingine hakutabadili chochote badala yake wakae na Baraza la Michezo la Taifa na Viongozi  wa chama cha waandishi kuifanyia maboresho katiba ili iendane na wakati na kila mwaandishi atoe mawazo yake kuimarisha chombo hicho.

“Mna uhuru wa kuunda chombo kingine siyo lazima taswa pekee ambao wamekaa kimya, lakini kuunda chombo kingine hakutasaidia kitu, kaeni na BMT mrekebishe katiba, mchague viongozi wengine na tunahitaji chombo imara,”alisisitiza Dkt. Mwakyembe.

Aliongeza kuwa, Waandishi wa habari za michezo wana umuhimu mkubwa sana kwa Taifa akirejea mashindano makubwa ya ‘AFCON’ yanayotarajiwa kufanyika nchini ambayo yataingiza mapato mengi kupitia sekta mbalimbali ikiwemo utalii ambapo alieleza kuwa waandishi ndio wenye mchango mkubwa wa kutangaza utalii wetu kupitia michezo hiyo.

“Tunawahitaji sana ndiyo maana nimeona tukae, bila nyie hakuna kitakachofanyika, kuna mashindano makubwa yanakuja mnahitajika sana,”alisisitiza Waziri.

Waziri Mwakyembe ameelekeza Baraza kulisisimamia mapema suala la marekebisho ya katiba ya chombo hicho na kuagiza uchaguzi kufanyika ndani ya mwezi Desemba.

 

 

 

1,336 total views, 3 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email14
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/10/02/dkt-mwakyembe-bmt-waiteni-taswa-na-wawakilishi-wa-waandishi-pitieni-katiba-ifanyiwe-maboresho-kabla-ya-kuelekea-katika-uchaguzi/">
RSS