DKT. MWAKYEMBE ALIPONGEZA BARAZA LA 14 KWA KUANZA AWAMU YAKE VIZURI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison George Mwakyembe amelipongeza Baraza la Michezo la Taifa (14) kuanza kazi vizuri kwa kuandaa Mkutano na Viongozi wa Vyama vya Michezo vya Taifa kuweka mikakati ya pamoja katika kuendeleza michezo nchini.

Dkt. Mwakyembe amelipongeza Baraza leo tarehe 10 Octoba, 2018 kwa kuanza kazi vizuri alipoalikwa kufungua Mkutano wao na Viongozi wa Vyama vya Taifa, mkutano ulioandaliwa kwa ajili ya kufanya tathmini ya ushiriki wa baadhi ya michezo katika mashindano ya kimataifa na kupanga mikakati ya maendeleo ya michezo kwa ujumla.

IMG_1441“BMT mmefanya vizuri kwa kweli kuandaa mkutano huu wa kukutana na Viongozi wa Vyama zaidi ya 30 ili kufanya tathmini na kuandaa mikakati ya pamoja kuendeleza michezo nchini,”alisema na kuongeza kuwa.

“Kuwaita wadau hawa muhimu katika maendeleo ya michezo ni kitu chenye afya sana mimi nawatakia kila la kheri,”alisema Waziri Mwakyembe.

Aidha, Waziri Mwakyembe amemwagiza Msajili kufanya uhakiki wa Mashirikisho/Vyama na Vilabu ambavyo vimesajiliwa na kuvifuta vyote ambavyo havina usajili na baada ya miezi sita (6) amletee orodha mpya ya Mashirikisho, Vyama na vilabu ambavyo vipo kisheria.

Hata hivyo Dkt. Mwakyembe amewataka Viongozi wa Mashirikisho na Vyama vyenye hadhi ya kuitwa hivyo wanazingatia uwepo wa Ofisi ili iwe rahisi kuwapata na hata wafadhili kuwaamini, lakini pia kuwa na Akaunti ya Benki kwa ajili ya kuweka pesa wanazopata kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo kwa wafadhili siyo kuweka katika akaunti binafsi pamoja na kuwa na Mpango kazi kwani bila hiyo si rahisi kupangilia rasilimali chache wanazopata.

IMG_1422Aliendelea kuwa, kulipa ada ni suala la kisheria ili kuonesha uhai wa Shirikisho au Chama, lakini suala la kuibua vipaji vya wanamichezo suala ambalo wameiachia Serikali kupitia michezo ya Shule za Sekondari (UMISSETA) na Shule za Msingi (UMITASHUMTA) wakati Mashirikisho na Vyama vinatakiwa kushirikiana na Serikali kuibua vipaji na kulitaka Baraza la Michezo kulisimamia hilo kwa karibu.

“Suala la kuibua vipaji wameiachia Serikali kupitia UMISSETA na UMITASHUMTA lakini Mashirikisho na Vyama wamejisahau katika hili, BMT simamieni hili ili tulete mapinduzi katika maendeleo ya Michezo,”alieleza Waziri Mwakyembe.

Lakini pia Dkt. Mwakyembe ameyasisitiza Mashirikisho na Vyama vya Michezo kuwa na Utawala bora kwa kubadilishana vipindi vya uongozi kwa kufanya chaguzi kulingana na Katiba zao pamoja na viongozi kujiepusha na rushwa kwani inadidimiza maendeleo ya michezo.

IMG_1616Kwa upande wake mwakilishi wa viongozi wa vyama vya michezo na  Mwenyekiti wa Chama cha mchezo wa Volleball Tanzania (TAVA) Meja Jenerali mstaafu Patrick Mlowezi amelishukuru sana Baraza kuandaa mkutano huo na kuomba waendelee kukutana na wadau hao ili kuimarisha maendeleo ya michezo nchini, na kumweleza Mheshimiwa Waziri kuwa, watayatekeleza maagizo yake.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa BMT Leodiger chilla Tenga alimweleza Dkt. Mwakyembe kuwa kwa kushirikiana na watendaji wa Baraza kwa ujumla wake watasimamia maagizo yake na kuhakikisha yanatekelezeka ndani ya kipindi alichoagiza cha miezi sita huku akiwaeleza viongozi hao kuwa Baraza litaendelea kukutana na wadau wake wakati wowote na milango ya BMT iko wazi muda wote kwa ajili ya kuwasikiliza wadau wake ili michezo iweze kulitangaza Taifa vyema.

 

 

 

 

 

 

104 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by EmailO
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/10/10/dkt-mwakyembe-alipongeza-baraza-la-14-kwa-kuanza-awamu-yake-vizuri/">
RSS