MTAONA MABADILIKO MWAKA KESHO VIWANJA AMBAVYO HAVINA HADHI YA KUCHEZEA LIGI KUU TUTAVIZUIA KUCHEZEA.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison George Mwakyembe ameeleza kuwa, ataongea na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wahakikishe mabadiliko yanafanyika mwakani katika viwanja mbalimbali vya soka nchini hasa vinavyotumika kuchezea ligi mbalimbali ikiwemo ligi kuu Tanzania Bara na mwaka 2020 hata ligi daraja la kwanza, visipofanyiwa maboresho Serikali itazuia ligi hizo kuchezewa katika viwanja hivyo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison George Mwakyembe akiwa ameongozana na viongozi mbalimbali wa uwanja wa Azam wakimpitisha sehemu tofauti tofauti za uwanja huo baada ya Mhe. Waziri kufanya ziara katika uwanja huo ambao utatumika mwakani kwa ajili ya michuano ya AFCON U17 2019.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison George Mwakyembe akiwa ameongozana na Kaimu Katibu wa BMT pamoja na viongozi mbalimbali wa uwanja wa Azam wakimpitisha sehemu tofauti tofauti za uwanja huo baada ya Mhe. Waziri kufanya ziara katika uwanja huo ambao utatumika mwakani kwa ajili ya michuano ya AFCON U17 2019.

Hayo ameyasema tarehe 11 Oktoba,2018 alipofanya ziara katika kiwanja kinachomilikiwa na kampuni ya Azam “Azam Complex” ambacho ni moja kiwanja kitakachotumika katika michuano ya “AFCON U17” ili kuona marekebisho yaliyofanyika katika kiwanja hicho kuelekea mashindano hayo mwakani  kufuatia maelekezo waliyopewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ili kupewa hadhi ya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ambao Viongozi wake watakuja kukagua mwezi Disemba viwanja vitakavyotumika kwa michuano hiyo 2019 nchini.

“Mtaona mabadiliko mwaka kesho, nitakaa na wenzetu wa TFF viwanja ambavyo havina hadhi ya kuchezea Ligi kuu na mwaka unaofuatia hata ligi daraja la kwanza visipofanyiwa marekebisho tutavizuia kuchezea ligi hizo,”alisema Mhe. Waziri.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison George Mwakyembe akionyeshwa ubora wa uwanja wa Azam na Mkandarasi wa Uwanja huo Victor Ndozero(aliyeinama chini mwenye tisheti ya Bluu) wakati alipofanya ziara kwenye uwanja huo kujiridhisha na maandalizi na maboresho ya viwanja kuelekea michuano ya AFCON U17, ambayo Tanzania ndio mwenyeji wa mashindano hayo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison George Mwakyembe akionyeshwa ubora wa uwanja wa Azam na Mkandarasi wa Uwanja huo Victor Ndozero(aliyeinama chini mwenye tisheti ya Bluu) wakati alipofanya ziara kwenye uwanja huo kujiridhisha na maandalizi na maboresho ya viwanja kuelekea michuano ya AFCON U17, ambayo Tanzania ndio mwenyeji wa mashindano hayo.

“Lazima kama Mkoa unataka kuvutia watu, hii ni biashara unapovutia timu nyingi kuja kwako, unavutia watu, kuna biashara ya chakula, mahoteli, na mambo mengi mazuri, kama hutaki wataenda sehemu nyingine, na ndio maana mimi nikishatamka hivi watu kama Iringa watakesha usiku kuboresha kiwanja chao ili timu zote kusini ziende kwao,”alieleza.

Katika ziara hiyo Dkt. Mwakyembe aliridhishwa sana na maboresho ya  miundombinu  ya uwanja wa Azam na kueleza kuwa  yamekamilika kwa asilimia 85 na anaimani kuwa sehemu iliyobaki itakamilika kabla ya kufika Disemba ambapo Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) litakapokuja kukagua.

IMG_1788Hata hivyo, Dkt. Mwakyembe ameeleza kuwa, pesa ya kufanya maboresho ya Viwanja vya Serikali ikiwemo kile cha Taifa na Uhuru imeshatoka na Makandarasi mchina aliyevijenga ataendelea na maboresho hayo ili kwenda na wakati ambao CAF wanataka.

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mashindano ya nchi za Afrika yajulikano kama (AFCON U17) yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2019 na Viwanja vyenye hadhi ya kutumika katika michuano hiyo ni Uwanja wa Taifa, Uhuru na Azam Complex ambavyo Mhe.Mwakyembe anahangaika viboreshwe kulingana na mahitaji ya michuano hiyo.

 

 

133 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by EmailO
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/10/11/mtaona-mabadiliko-mwaka-kesho-viwanja-ambavyo-havina-hadhi-ya-kuchezea-ligi-kuu-tutavizuia-kuchezea/">
RSS