VIONGOZI WAPYA OBFT KUPATIKANA DISEMBA 1

Moja ya pambano la ngumi za wazi
                                                           Moja ya pambano la ngumi za wazi

 

Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limetangaza Uchaguzi wa Shirikisho la Ngumi za Wazi Tanzania (OBFT) unaotarajiwa kufanyika tarehe 1 Disemba, 2018 katika moja ya kumbi za Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Fomu zitaanza kutolewa katika Ofisi za Baraza zilizopo Uwanja wa Taifa, na  katika tovuti ya Baraza ambayo ni www.nationalsportscouncil.go.tz, kuanzia tarehe 25 Oktoba huku mwisho wakuchukua na kurudisha  fomu hizo ikiwa ni tarehe 27 Novemba, 2018. Wakati usaili wa wagombea wa nafasi tofauti ukitarajiwa kufanyika Novemba 30 siku moja kabla ya uchaguzi huo.

Aidha, nafasi zinazogombewa katika uchaguzi huo ni nafasi ya Rais na Makamu wake,     Katibu Mkuu na Msaidizi wake, na Mweka hazina huku ada ya fomu kwa nafasi hizo ikiwa ni shilingi laki mbili za kitanzania (200,000).

Zingine ni nafasi tisa (9) za wajumbe wakuchaguli ikiwemo ya Mjumbe wa kamati ya Walimu, Mjumbe wa kamati ya Waamuzi na Majaji, Mjumbe wa kamati ya Ufundi, mjumbe wa kamati ya Mashindano na Vifaa, Mjumbe wa kamati ya Wanawake na Vijana, Mjumbe wa kamati ya Maendeleo ya Mikoa na Taasisi za Umma, Mjumbe kamati ya Mipango na Fedha, na Mjumbe wa kamati ya Afya.

Mjumbe mwingine katika uchaguzi huo ni yule anayehusika na kamati ya ngumu za kulipwa za Shirikisho la ngumi za Wazi LA Dunia ‘AIBA’ (AOB), ngumi za kulipwa AIBA (APB), vilevile atahusika katika ligi za ngumi za dunia (WSB), ambapo ada ya fomu kwa nafasi hizo za wajumbe ikiwa ni Shilingi elfu hamsini (50).

Sifa za wagombea ni pamoja na kuwa raia wa Tanzania, kuwa hajawahi kuliongoza Shirikisho kwa awamu mbili mfululizo (yaani miaka minane), hajawahi kupatikana na hatia ya kosa la jinai katika Mahakama yoyote Tanzania, elimu isiyopungua kidato cha nne kwa nafasi za juu, nafasi ya Mweka hazina awe na elimu ya uhasibu kuanzia ngazi ya cheti nakuendelea huku nafasi za ujumbe Katiba ya OBFT ikimtaka mwenye kujua kusoma na kuandika na awe amewahi kuucheza mchezo huu katika kipindi kisichopungua miaka mitano.

Sifa zingine ni mgombea awe hajawahi kucheza, kuongoza au kuratibu mchezo wa ngumi za kulipwa katika ngazi yoyote, awe ameisoma na kuielewa katiba ya OBFT pamoja na kutokuwa mchezaji wa ngumi.

Wagombea wanatakiwa kulipia fomu katika akaunti ya Baraza kwa jina la National Sports Council Ac. No. 20401100013 na kuwasilisha BMT risiti ya Benki na fomu zilizojazwa kwa usahihi.

Aidha, Baraza limetoa wito kwa wenye nia ya dhati ya kuuendeleza na kuiletea sifa nchi kupitia mchezo huu kuwahi mapema kuchukua fomu na kuwania nafasi atakayoitendea haki.

 

654 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/10/24/viongozi-wapya-obft-kupatikana-disemba-1/">
RSS