MTENDAJI MKUU BMT ASISITIZA KILA MTUMISHI KUIPENDA KAZI YAKE

Kaimu Katibu Mkuu wa BMT Makoye Alex Nkenyenge akieleza jambo kwa Watumishi (hawapo pichani) wakati wa kikao cha watumishi wa baraza Octoba 25 jijini Dar es salaa.
Kaimu Katibu Mkuu wa BMT Makoye Alex Nkenyenge akieleza jambo kwa Watumishi (hawapo pichani), pembeni ni Kaimu Meneja wa Utawala na Rasilimali watu  Jamila Mongi wakati wa kikao cha watumishi wa baraza Octoba 25 jijini Dar es salaa.

 

Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Makoye Alex Nkenyenge amewasisitiza Watumishi wa Baraza kila mtu kuipenda kazi yake kwani ndiyo kinachoonesha uwepo na ukuuwaji wa Taasisi na kuacha kukata tamaa kwakuwa kunawafanya watumishi kutoipenda kazi ambako kunaididimiza Taasisi.

Rai hiyo ameitoa tarehe 25 Octoba, 2018 wakati wa kikao cha Wafanyakazi wa Baraza ambacho moja ya agenda za kikao hicho  ni taarifa ya kikao cha Msajili wa Hazina na Taasisi zaidi ya 70  Octoba 2 pamoja Maagizo ya Rais kwa BMT  wakati alipokutana na Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) baada ya mechi yao timu ya Taifa ya Cape Verde.

“Kazi ukiwa nayo ndiyo unaichukia, tuache kukata tamaa kwani ndiko kunapelekea kuzichukuia kazi zetu,”alisema Nkenyenge.

 

IMG_3002IMG_2961

 

Watumishi wa BMT wakiwa makini kumsikiliza Mtendaji Mkuu mbele Alex Nkenyenge wakati wa kikao cha wafanyakazi

 

Aliendelea kuwa, mambo ambayo mnatakiwa kama watumishi kuzingatia ni utawala bora kuanzia ngazi ya juu hadi chini kwa kuimarisha uwajibikaji, ushirikiano, kukamilisha mkataba wa huduma kwa wateja na usimamizi wa rasilimali za Umma nani katika masuala muhimu aliyoelekeza Msajili wa Hazina.

Awali,  Nkenyenge alieleza kuwa, katika kikao na timu ya Taifa Mhe.Rais amesisitiza Baraza kuvisimamia vyama vya michezo na taasisi zinazoendesha michezo kuzingatia Sheria na kanuni zinazoendesha michezo na kuiepuka kutoa au kupokea rushwa.

88 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/10/25/mtendaji-mkuu-bmt-asisitiza-kila-mtumishi-kuipenda-kazi-yake/">
RSS