MTAALAMU WA RIADHA AWASILILI KUONGEZA NGUVU YA WATANZANIA KUWAKILISHWA NA WACHEZAJI WENGI 2020 OLYMPIKI

Mwalimu wa Mchezo wa riadha kutoka nchini Japan Ayane Sato atakayekuwa nchini kwa miaka miwili akiwaandaa wanariadha wa Tanzania kufikia viwango vya Olimpiki 2020 katika mbio fupi na za kati.
Mwalimu wa Mchezo wa riadha kutoka nchini Japan Ayane Sato atakayekuwa nchini kwa miaka miwili akiwaandaa wanariadha wa Tanzania kufikia viwango vya Olimpiki 2020 katika mbio fupi na za kati.

Mwalimu wa riadha amewasili nchini akitokea nchini Japan kupitia Taasisi ya ushirikiano wa kimataifa ya Japan (JICA) ambaye atafanya kazi Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kupitia Shirikisho la riadha Tanzania (RT) kwa kipindi cha miaka miwili (2) ambapo, atawafundisha wanariadha wengi waliopo katika taasisi tofauti zinazojihusisha na mchezo huo ili kukidhi vigezo vya kushiriki mashindano ya Oliympiki 2020 yanatarajiwa kufanyika nchini Tokyo Japan.

Mtaalamu huyo wa riadha ametambulishwa tarehe 15 Novemba, 2018 na Viongozi wa  Shirikisho la riadha Tanzania katika mkutano na waandishi wa habari za michezo uliofanyika katika moja ya ukumbi wa Taifa Jijini Dar es salam.

Akiongea katika mkutano huo Katibu  Msaidizi wa RT Ombeni Zavala wakati akimtambulisha mtaalamu huyo ajulikanaye kwa jina la Ayane Sato, alieleza kuwa, mtaalamu huyo atashirikiana na walimu wa mchezo huo waliopo nchini lakini yeye atajikita katika mbio fupi na mbio za kati ambazo nchi yetu imekuwa inakosa timu nzuri ya kushiriki mashindano ya Kimataifa na kukosa matokeo mazuri.

 

Katibu Mkuu Msaidizi wa Shirikisho la Riadha Tanzania Ombeni Zavala (kulia) akiongea na Waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kumtambulisha Mkufunzi wa mchezo wa riadha kutoka Japan atakayeanza kufanya kazi mwishoni mwa mwezi Novemba na atakuwepo kwa miaka miwili kuwaandaa wanariadha wa mbio fupi na za kati pamoja na mtupo na miruko, kushoto ni Mkufunzi huyo Ayane Sato.
Katibu Mkuu Msaidizi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Ombeni Zavala (kulia) akiongea na Waandishi wa habari wakati wa mkutano nao kumtambulisha Mkufunzi wa mchezo wa riadha kutoka Japan atakayeanza kufanya kazi mwishoni mwa mwezi Novemba na atakuwepo kwa miaka miwili kuwaandaa wanariadha wa mbio fupi na za kati pamoja na mitupo na miruko, kushoto ni Mkufunzi huyo Ayane Sato.

Mama Zavala aliongeza kuwa, nchi ya Japan kupitia Taasisi ya JICA imekuwa na mahusiano na ushirikiano mzuri na nchi yetu katika mchezo wa riadha  kwa miaka miwili sasa ambapo, mwaka jana walianza na mashindano ya wanawake ambayo yalifanyika kwa mafanikio mazuri lakini pia washindi walishiriki mwaka huu katika mashindano ya riadha Mjini Nagai nchini humo ambapo wanariadha wetu walifanya vizuri.

“Nchi ya Japan kupitia Taasisi yake iliopo nchini ya JICA imekuwa na mahusiano mazuri sana katika mambo mbalimbali na kuendeleza michezo ukiwemo huu wa riadha ambapo kwa miaka miwili sasa wamedhamini mashindano ya wanawake kwa mafanikio makubwa na washindi wameenda katika mashindano Mjini Nagai na wamefanya vizuri sana kwa kurudi na medali,”alisema na kuongeza;

“Pia mwezi huu Novemba,  24 na 25 yatafanyika tena mashindano ya riadha ya wanawake ambapo  Mikoa zaidi ya 27 imethibitisha ushiriki wa wanariadha wa kike na washindi watapata tena nafasi ya kwenda Nagai kwenye mashindano yao ili kuimarisha viwango vya wachezaji wetu, tunaimani kubwa 2020 tutakuwa na wawakilishi washindani wengi,” alieleza Mama Zavala.

Awali Msemaji wa RT Tulo Chambo alisema Sato atatoa mafunzo yake kupitia shule mbalimbali ikiwemo Shule ya Sekondari Makongo, Jitegemee, Filbert Bayi, Load Buden Kipingu na zingine atakazoelekezwa pamoja na kutoa mafunzo katika chuo cha Wizara yenye dhamana ya michezo Malya.

Kwa upande wake, Mkufunzi huyo Ayane Sato amesema yeye yuko tayari kufanya kazi kwa uwezo wake wote kuhakikisha wanariadha wengi wa Tanzania wanapata vigezo na kufanya vyema katika mashindano ya Olympiki yanayotarajiwa kufanyika nchini kwao mwaka 2020.

 

1,421 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email4
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/11/15/mtaalamu-wa-riadha-awasilili-kuongeza-nguvu-ya-watanzania-kuwakilishwa-na-wachezaji-wengi-2020-olympiki/">
RSS