WAZIRI MWAKYEMBE AKAGUA BAO LILILO ANDALIWA NA SHIMBATA KUMUENZI MWALIMU NYERERE NA UTAMADUNI WA KITANZANIA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akitoa maelekezo kwa Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Bao Tanzania Monday Likwepa mbele ya Waziri kuhusu bao hilo linalotaka kukabidhiwa kwa Rais John Magufuli siku ya Uzalendo mwisho wa wiki jijini Dodoma.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akitoa maelekezo kwa Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Bao Tanzania Monday Likwepa mbele ya Waziri kuhusu bao hilo linalotaka kukabidhiwa kwa Rais John Magufuli siku ya Uzalendo mwisho wa wiki jijini Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harisson G. Mwakyembe leo amekagua Mabao yaliyoandaliwa na Shirikisho la Mchezo wa Bao Tanzania (SHIMBATA) kwa lengo la kumkabidhi Mhe. Rais John Magufuli siku ya Uzalendo inayotarajiwa kufanyika mwisho wa wiki Jijini Dodoma wakiwa na Imani kuwa ni Rais Mzalendo na anayeamini utamaduni wa nchi yake kama alivyokuwa Hayati Mwalimu Nyerere aliyekuwa anaupenda sana mchezo wa bao.

Mheshimiwa Mwakyembe amekagua mabao hayo katika Ofisi za Baraza la Michezo zilizopo uwanja wa Taifa ili kujiridhisha na viwango vya mabao hayo kabla ya kupelekwa kwa Mheshimiwa Magufuli na kuwataka waandae utaratibu mapema wa kuyasafirisha kuelekea Dodoma.

Mwenyekiti wa BMT Leodiger Tenga aliyekaa akieleza jambo kwa viongozi wa Shimbata alipokuwa akioneshwa bao na Rais wa Shirikisho hilo.
Mwenyekiti wa BMT Leodiger Tenga aliyekaa akieleza jambo kwa viongozi wa Shimbata alipokuwa akioneshwa bao na Rais wa Shirikisho hilo.

Aidha, Mhe. Waziri amemtaka Rais wa Shirikisho hilo Monday Likwepa kutafuta wadhamini wa mchezo huo ili waweze kuueneza kwa watanzania wengi zaidi ili waweze kuukuza utamaduni na kuwa wazalendo kwa kuipenda michezo yao.

“Tafuteni wadhamini wa mchezo huu ili uweze kuwafikia watanzania wengi na hatimaye wakuze utamaduni na uzalendo wa michezo yao,”alisema Waziri.

Kwa upande wake Rais wa Shimbata Monday Likwepa alisema miaka ya 1963 Mwalimu Nyerere alimfundisha Rais wa China Hayati Mao Tse Tung mchezo wa bao na akatamani ukafundishwe nchini kwake lakini halikufanyika  hilo, hivyo Bao la pili ni kwa ajili ya kumpa Rais wa china Xi Ji Ping na kumwomba Rais wetu amkabidhi bao hilo na amwombe mchezo   wa bao ukafundishwe nchini China ili tuzidi kuueneza katika mataifa mengine.

 

7 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/12/05/waziri-mwakyembe-akagua-bao-lililo-andaliwa-na-shimbata-kumuenzi-mwalimu-nyerere-na-utamaduni-wa-kitanzania/">
RSS