NKENYENGE: KUMBUKENI KUITEKELEZA KATIBA YENU NA MAELEKEZO YALIYOTOLEWA NA BMT

Kaimu Katibu Mtendaji wa BMT kulia Alex Nkenyenge akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa OBFT baada ya kuapishwa, kulia ni Wakili Innocent P. Mwelelwa
Kaimu Katibu Mtendaji wa BMT Alex Nkenyenge kulia akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa OBFT baada ya kuapishwa, kulia ni Wakili Innocent P. Mwelelwa

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Alex Nkenyenge amewataka Viongozi wa Shirikisho la Ngumi za Wazi Tanzania (OBFT) kukumbuka kuyatekeleza majukumu yao kwa kufuata katiba na maelekezo  yaliyotolewa na Baraza kwa vyama vyote ili kufikia malengo ya maendeleo ya michezo nchini.

Hayo ameyasema leo tarehe 07 Disemba, 2018 baada ya kuapishwa kwa viongozi wa shirikisho hilo waliochaguliwa tarehe 01 mwezi huu ili kulitumikia shirikisho hilo kwa kipindi cha miaka minne (4) kwa mujibu wa Katiba yao.

“Yapo majukumu ya msingi ya kutekeleza kulingana na Katiba ya shirikisho na Sheria ya BMT lakini bila kusahau maelekezo yaliyotolewa na Baraza kwa vyama vyote vya michezo ili kuyafikia malengo ya maendeleo ya michezo nchini,”alisema Nkenyenge.

Maelekezo yaliyotelewa na Baraza la michezo ni Chama au Shirikisho kuwa na Ofisi inayoeleweka, kuwa na akaunti ya chama ili wanapopata ufadhili pesa ya chama isiingie katika akaunti binafsi. Lakini pia kuwa na mpango kazi ili kufahamu wanafanya nini, wapi, kwa kiasi gani na kwa wakati gani na vilevile  kuimarisha utawala bora.

Lakini pia viongozi hao wamesisitizwa kukumbuka michezo ni zaidi ya kujitoa, hivyo wajue namna ya kuwatumia wanachama wao ili waweze kusaidia shirikisho kwa kuchangia na hata wao kuchangia kwa namna moja au nyingine badala ya kufikiria kufaidika wao.

“Michezo ni zaidi ya kujitoe, mjue namna ya kuwatumia wanachama wenu ili waweze kulichangia shirikisho,”alieleza Nkenyenge.

Viongozi walioapishwa ni Rais wa OBFT Muta Rwakatare, Makamu wake Andrew Mhoja, Katibu Mkuu Lukelo A. Willilo, na Wajumbe ni Zainabu Mbonde, Mohamed Abubakar, Mohamed Kasilamatwi, Riadha Kimweri na Mafuru M. Mafuru.

Aidha, viongozi hao wameagizwa kuhakikisha wanaitisha uchaguzi mdogo ili nafasi zilizokosa wagombea kupata watendaji wake mapema ikiwemo ya Katibu Msaidizi, Mjumbe wa wanawake, mjumbe anayeshughulikia tiba na nafasi ya mweka hazina.

 

 

141 total views, 1 views today

Fuatilia Mchezo, like:
0

Leave a Reply

Michezo ni yetu wote, fuatilia, Wataarifu wengi

Follow by Email5
Facebook
Facebook
YouTube0
YouTube
Google+0
Google+
http://nationalsportscouncil.go.tz/blog/2018/12/07/nkenyenge-kumbukeni-kuitekeleza-katiba-yenu-na-maelekezo-yaliyotolewa-na-bmt/">
RSS